
Macho ya watu wengi katika shindano la Big Brother yameanza kushuhudia
vijimambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na love scenes zilizochukua nafasi
usiku wa kuamkia leo kwa washiriki wawili walioanza kuashiria hali ya
kutengeneza ukaribu wa kufahamiana and plus!Usiku wa kuamkia leo (May
29) wakati washiriki wengine wakiwa wameshalala, ‘Bolt’ ya Bolt ambaye
ni mshiriki wa kiume anaeiwakilisha Sierra Leone ilionekana kuanza
kuifunga ‘nati’ ya Betty mshiriki wa kike kutoka Ethiopia ambao
walionekana kuwa na ukaribu wa faragha ulithibitisha kuwa wamesha
bonyeza button ya uhusiano wa kimapenzi. Washiriki hao wote wako Diamond
House ambayo mkuu wake ni Feza Kessy kutoka Tanzania.
Bolt na Betty waliofahamiana Jumapili iliyopita walishindwa kuficha
mahaba yao mapya baada ya kuonekana wakiacha mikono yao kufanya kazi
zaidi kwa kushikana kimahaba, na lips zao kusalimiana wa kisses gizani
wakati wenzao wakiwa fofofo, na baadae kulala wakiwa wamekumbatiana huku
Betty akiwa amemlalia Bolt Kifuani na mkono wake kuuingiza ndani ya
t-shirt yake.

