Jana
ikiwa ni birthday ya mtoto mzuri na 'Hakuna Yule' hit maker wa Ogopa
Djs ya Kenya Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril, alitua jijini dar es
salaam leo na sababu ya ujio wake ni vitu vikubwa viwili.
Akihojiwa katika kipindi cha
XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni
ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch
single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko
ziarani barani Ulaya, party itakayofanyika usiku wa leo (April 30) pale
Elements club.
Kuhusiana na maneno ambayo
yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na
Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho,
Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa
kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond we are
just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika
muziki", alisema Avril.
Kama ulikuwa hujui hii ndio
birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote
zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.
Jana Avril ametimiza miaka 26,alizaliwa April 30, 1986 huko Nakuru Kenya.
we wish you a happy birthday Avril na karibu sana Tanzania



