Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Wednesday, May 29, 2013

ANGALIA PICHA ZA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MZUMBE WAANDAMANA USIKU KWENDA KWA MKUU WA MKOA


Wanafunzi wa shule ya  serikali ya Mzumbe Sekondari jana saa nane usiku wameandamana kutoka shueleni kwao wakieleke ofisi ya mkuu wa mkoa  wakishinikiza serikali ya mkoa wa Morogoro kuwatimua walimu wao watano akiwemo mkuu wa shule hiyo wakiwashutumu kwa vitendo mbali mbali ikiwemo vya ufisadi.Wanafunzi hao walizuiwa na askari eneo la Mindu  saa 12 alfaji ya  na kwamba kwa umoja wao madent hao waligoma kutoka barabnara mpka mkuu wa mkoa au katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro kufika kwenye eneo hilo na kusikia kilio chao.

Katibu Tawala wa mkoa huo Bw.Elias Ntandu kwa kushirikiana na Afisa  Elimu wa mkoa wa Morogoro Bi Wariambora Nkya na viongozi mbali mbali wa halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mvomero ilipo shule hiyo waliufika kwenye eneo la  Mindu na kusikiza malalamiko ya wanafunzi hao.Akizungumza kwa niaba ya wenzeke kiongozi wa wanafunzi hao Bw Emily Mayani aliueleza uongozi huo wa serikali ya mkoa kwamba hawata rudi shule mapka serikali itakapo watimu walimu watano akiwemo mkuu wa shule hiyo Bw Dismas Njawa.na msaidizi wake Bw Mtalasi.





Walimu wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mwalimu wa malezi wa shule hiyo Edwin Matenga,mwalimu wa nidhamu Mohamed Soni na mwalimu wa taaluma Gasbert Rwegasira,kwa mujibu wa wanafunzi hao hao walimu hao waliowaita Top 5 wanawashutumu kwa mambo mbali mbali ikiwemo ya ufisadi na lugha za matusi kwa wanafunzi.


Viongozi wetu michango jambo moja kuwafukuza mara moja walimu hao kutufukuza sisi wanafunzi 60 ambao asilimi 90 wazazi wetu ni wakulima mfano mimi wazazi wangu ni wakulima wa nyanya,hatuwezi kuvumilia uongozi unatumia shilingi milioni 50 kupaka rangi chumba kimoja tukio hoji tunaambia sisi watoto wadogo na kwamba kama tunataka twenda kukasoma shule ya wasichana ya kilakala hayo si matusi makubwa, mbali na ufisadi huo baa imejengwa eneo la shule yetu wakati sheria za nchi zinatuzuia wanafunzi kukaa au kuingia baa"alisema kiongozi huyo wa wanafuzni wa shule hiyo kwa jazba kubwa.


Uongozi wa serikali hiyo ya mkoa uliwaomba wanafunzi hao kuwa watulivu na kuahdi kuyafanya kazi mapendekezo hayo waliyotoa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...