Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Saturday, May 4, 2013

ALIYEUA ASKARI POLISI MANYARA AKAMATWA

720 akili mpwapwa
Jeshi la polisi Mkoani Manyara linamshikilia mfanyabiashara wa madini
ya Tanzanite,Lawi Abayo (33) kwa kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi
askari polisi wa kituo cha Mirerani Wilayani Simanjiro G.7037 Joseph
Tairo (28).

Akithibitisha kushikiliwa kwa mfanyabiashara huyo,Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara,Kamishna Msaidizi Akili Mpwapwa alisema jana kuwa Abayo alijisalimisha juzi kwenye kituo cha polisi wilayani Babati.
Kamanda Mpwapwa alisema baada ya mfanyabiashara huyo kujisalimisha mwenyewe hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mtuhumiwa huyo Mahakamani ili kujibu shtaka la mauaji.
“Ni kweli tunamshikilia Abayo ambaye alijisalimisha mwenyewe kwa kuja polisi,baada ya kuona kuwa hawezi kushindana na mkono wa Serikali ambayo ni mrefu,” alisema Kamanda Mpwapwa.
Hata hivyo,Kamanda Mpwapwa alithibitisha kushikiliwa kwa bastola inayodaiwa kutumiwa na mfanyabiashara huyo kumuua Tairo na pia wanalishikilia gari aina ya Prado alilotumia kutorokea mara baada ya tukio hilo.
Askari huyo PC Tairo alifariki dunia Aprili 15 mwaka huu,kwenye hospitali ya Muhimbili (Moi) baada ya kupigwa risasi ya kichwa na kujeruhiwa Aprili 7 akiwa kazini mjini Mirerani na kuzikwa kijijini kwao Kaboro,Mkuu Rombo Aprili 19.
Chanzo cha tukio hilo ni PC Tairo akiwa na askari mwenzake G.8523 PC Martin,kumkamata mhalifu mmoja na wakati wakimpeleka kituoni ndipo mfanyabiashara huyo akazuia zoezi hilo kwa kumpiga risasi askari huyo.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...