STAA wa
filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kutupiwa nje na
baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya kupanga
aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es salaam.
Jacqueline Wolper Massawe.
Madai hayo
yalitua kwenye dawati la GPL hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu
hiyo ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa
kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh.
milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu
wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake
kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina
tunalo), aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa
kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.
“Wolper
alipopigiwa simu alikuja juu na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama
anamfuatilia eti atamfunga kama mume wa mama huyo alivyofungwa na
kumwambia kuwa atampelekea polisi wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo
aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama
huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina
moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Baada ya
kujazwa data hizo, GPL ilifanya jitihada za kumsaka Wolper na
alipopatikana alisema kuwa hajawahi kudaiwa na huyo mama na anayesema
hivyo huenda alimuona wakati anahamisha vitu vyake kwani kwa sasa
amehama kwenye nyumba hiyo.
Mwandishi
wetu hakuishia hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa
kwa jina moja la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba
suala hilo lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya
kufanya usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa
Nyumba Kumi, Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili
kuzungumzia sakata hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema
kuwa msanii huyo alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake
wakachukue vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba
aliwazuia mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu
vyake.
CREDIT:GPL



