Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, May 30, 2013

TAARIFA YA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE, UFAULU WAPANDA KWA ASILIMIA 23....YAANGALIE HAPA.


 

Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu.

Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57.

Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

 
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.

Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

KUPATA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE 2012

http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/CSEE_2012/olevel.htm
Read More >>

Wabunge wa Kenya wapata pigo

Mahakama nchini Kenya imesimamisha utekelezaji wa nyongeza ya mishahara ambayo wabunge wa nchi hiyo walipendekeza kujiwekea. Chama cha mawakili nchini Kenya kiliwasilisha ombi la kutaka kuwekewa amri ya kisheria wabunge hao siku moja baada ya wabunge hao kupiga kura ya pamoja kutaka wajoingezee mishahara.
 Wanaharakati wamekuwa wakipinga jaribio hilo huku 
wakiandaa maandamano katika barabara za jiji la Nairobi wakimuomba rais asiidhinishe kura hiyo.
Hapo jana Rais Uhuru Kenyatta aliwafokea wabunge hao kwa uamuzi wao huku akisema kuwa mishahara ya wafanyikazi wote wa Umma inadhibitiwa na tume ya mishahara iliyoundwa.
 Kwa upande wao wabunge hao wameishutumu tume hiyo wakidai kuwa ilivuka mpaka wake kupendekeza wapunguziwe mishahara yao kwa takriban asili mia hamsini kutoka dola elfu kumi kwa mwezi.
 Wabunge hao wameelezea hasira zao juu ya tamko la Rais Uhuru Kenyatta na tume ya kudhibiti mishahara ya maafisa wa serikali ambao wanasema waache vitimbi vyao vya kutaka kuongezwa mishahara.
 Wanatishia kubadilisha sheria ya idadi ya maafisa wanaoweza kuhudumu katika tume za serikali hadi watatu , kupunguza mishahara ya maafisa wa serikali kwa asilimia hamsini na saba na kuwaondolea wananchi wanaopata chini ya shilingi elfu hamsini kama ajira uwezo wa kutozwa kodi.
 Wabunge hao hata hivyo hawaoni ubaya wowote wa kulalamika kuwa mishahara yao inapunguzwa wakisema wanasubiri tume ya bunge kuwalipa mishahara yao ya laki nane na hamsini kutoka laki tano.
Read More >>

PICHA ZA MATUKIO YANAYOENDELEA AFRIKA KUSINI ULIPO MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA

Muonekano wa nje wa hospitali ya St Hellen Joseph, ulipokuwa mwili wa marehem Albert Mangwea
Millard akifanya mahojiano na mmoja wa watanzania walioko Soth Africa
Nje ya mochwari ya Serikali Hillbrow Johannesburg ulikohamishiwa mwili wa Ngwea ni Watanzania wakiongozwa na Kinje Ngomale Mwiru wakitazama sample ya majeneza mbalimbali ili wajue la kununua, hapa walikua na mfanyabiashara wa kampuni ambayo pia huwa inashughulika na kusafirisha miili ambapo gharama yake ni zaidi ya milioni nne na nusu.
Millard Ayo akifanya interview na mmoja wa Watanzania nje ya hospitali alikolazwa M2TheP.
Read More >>

KUTOKA KWENYE VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodomamay 30, 2013.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Mary Nagu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema wakiteta Bungeni Mjini Dodoma May 30,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, Bungeni mjini Dodoma, May 30,2013.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiataifa, Bernad Membe akisoma bajeti ya Wizara yake, Bungeni mjini Dodoma May 30, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, Bungeni mjini Dodoma May 30, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa,Bungeni Mjini Dodoma May 30,2013.
Mbunge wa Mwanza Mjini Ezekiel Wenje akiongozwa na Mbunge wa Mtera,Livingstote Lusinde (kushoto ) na Ofisi wa Bunge ( jina halikupatikana) kutoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya hotuba yaupinzani kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyokuwa akiisoma kupingwa na wabunge wa CUF, Bungeni mjini Dodoma May 30, 2013/ (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Read More >>

BIBI KIZEE WA MIAKA 65 AFARIKI DUNIA AGONGWA NA GARI,NI MMOJA KATI YA WALE WALIODHANIWA WACHAWI WALIOANGUKA MHONGOLO WILAYANI KAHAMA

BIBI MWAJUMA MPONI AKIWA HOI MARA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA MAJI

 


WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI SHIJA NKWABI (80) NA MWAJUMA MPONI (65).

Bibi huyo baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza vya maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala chini ya miti au chini ya magari yaliyopaki.
Kwa mujibu wa madreva wanaopaki magari yao eneo hilo wameiambia blog hii kuwa hata wao walishawahi kumkosa kumgonga mara nyingi katika eneo hilo.

MATUKIO KATIKA PICHA

ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA.

BIBI MWAJUMA AKIWA HOI BAADA YA KUKANYANGWA NA GARI

POLISI WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMPELEKA HOSPITALI BIBI HUYO

AISEEE INASIKITISHA SANA

MGUU WA KULIA WA BIBI HUYO UKIWA UMEKATIKA KABISA NA KUSHIKILIWA NA NGOZI TU


VIJANA WA KAHAMA MJINI WAKIWASADIA POLISI KUUPAKIA MWILI HUO KWENYE GARI.

BIBI MWAJUMA AKITEREMSHWA HOSPITALINI.
HAPA VIJANA WA KAHAMA WAKIMSUKUMA BIBI HUYO KUMUINGIZA HOSPITALINI ,TAFADHALI USINIULIZE MANESI NA MADAKTARI WALIKUWA WAPI KUTEKELEZA JUKUMU LAO.
VIJANA WAKIENDELEA KUJITOLEA KUMSAIDIA BIBI HUYO ILI AWAHI KUPATA MATIBABU,SWALI LANGU NI JE WANA UZOEFU WA KUSUKUMA WAGONJWA KATIKA MAGARI HAYO?
 
KAHAMA
Bibi mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwajuma Mponi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 75 hadi 80 amefariki dunia leo baada ya kukanyagwa na gari la maji taka wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wilayani Kahama, Gerge Simba, Bibi huyo amekanyagwa leo mchana maeneo ya nyuma ya hospitali ya wilaya hiyo wakati akiwa amelala chini ya gari hilo kwa ajili ya kivuli.
Simba amesema Bi Mwajuma amefariki dunia mida ya saa moja jioni leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana majeraha makubwa yaliyompata ikiwemo kuvunjika vibaya mguu wake wa kulia.
Hata hivyo Simba ametoa wito kwa madereva kuwa makini na kuhakikisha wanakagua chini magari yao sehemu wanapopaki au kupiga honi kabla ya kuondoka kwani ni hatari kwa wazee wanaokuwa wanajizuia jua na hata kwa watu wengine.
Amesema dereva wa gari hilo ambaye alikimbia kufuatia tukio hilo, kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya kukamatwa jioni hii maeneo ya Kahama mjini.
Kumbukumbu zimebaini kuwa Bibi huyo ni mmoja kati ya wale walioanguka April 3 katika kata ya Mhongolo wilayani Kahama na kupelekwa polisi kwa kudhaniwa kuwa ni wachawi.
Bibi huyo baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza vya maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala chini ya miti au chini ya magari yaliyopaki.
 
Credits: Kb blog
Read More >>

TAHADHARI YA UGONJWA WA NIMONIA INAYOTOKANA NA CORONA VIRUS

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) mnamo tarehe 22 Mei 2013, kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Nimonia unaosababishwa na kirusi cha “Novel Coronavirus”.Taarifa hiyo inaeleza kuwa,tangu ugonjwa huo utokee mwishoni wa mwaka 2012 hadi tarehe 23 Mei 2013  idadi ya wagonjwa wapatao 44 na vifo 22 viliripotiwa
Shirika la Afya Duniani limethibitisha ugonjwa huu kuwepo katika nchi za Mashariki ya Kati  yaani Jordan, Qatar, Saudi Arabi na Falme za Kiarabu (UAE). Katika bara la Ulaya, ugonjwa huu umethibitishwa kutokea nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza. Katika bara la Afrika, ugonjwa huu umetokea Tunisia.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi wote, katika mikoa yote ya Tanzania na hasa wale wanaosafiri kuelekea maeneo tajwa yenye uthibitisho wa ugonjwa huu.
Ugonjwa huu unaenezwa na kirusi kiitwacho “novel coronavirus (nCoV).”. Dalili kuu za ugonjwa huu ni kushindwa kupumua kwa ghafla, homa kali, kukohoa, na kubanwa na mbavu na hatimaye kupata Nimonia. Dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kupata maumivu makali ya tumbo pamoja na  kuharisha.
Vile vile ugonjwa huu unaweza kupelekea figo kushindwa kufanya kazi na hata kusababisha  kifo. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu ni kati ya siku 2 hadi 10 baada ya kupata maambukiziUgonjwa huu hauna tiba wala chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Njia za maambukizo bado hazijajulikana ingawa uwezekano mkubwa wa maambukizo ni kwa kwa njia ya hewa (kukohoa/kupiga chafya) au kwa kugusa majimaji/makamasi kutoka kwa mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:

·        Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania bara. Aidha, taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),  “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli ikiwa ni pamoja na vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.    

·        Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipakani. Aidha watalaamu hawa pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu na jinsi ya kujikinga na maambukizi ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.

·        Wizara inasisitiza kuwa hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili kwa wasafiri watakaokwenda au kurudi katika maeneo tajwa yaliyothibitishwa kuwa na ugonjwa huu. Vipeperushi vya ugonjwa huu vimetumwa katika maeneo ya mipakani ili iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.

·        Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya na mipakani wa  namna ya kutambua na kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa huu pamoja na uchukuaji wa sampuli iwapo mgonjwa atapatikana


·        Kupeleka vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya

Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyeripotiwa nchini. Wizara inapenda kutoa tahadhari kwa wananchi juu ya umuhimu wa KUNAWA MIKONO VIZURI KWA SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA na pia KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA AU KARATASI LAINI  WAKATI WA KUKOHOA AU KUPIGA CHAFYA.

Pia wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaja
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
30/05/2013
Read More >>

UPDATES: KUTOKA KAMATI KUU YA MAZISHI IMESEMA MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA UTAFIKA NCHINI TAREHE 1/06/2013

Marehemu Albert Mangwea enzi za uhai wake
 
Kwa ushirikiano na shirikisho la muziki Tanzania habari zinasema kwamba mwili wa marehemu Albert Mangwea unatarajia kuletwa nchini Tanzania tarehe moja (1)  mwezi wa sita 2013 (01/06/2013) ambayo itakuwa ni Jumamosi na kuna mpango wa kuandaa sehemu ya wapenzi na mashabiki kumuaga siku ya jumapili katika eneo litakalotangazwa na Kamati ya mazishi
Read More >>

ICHEKI VIDEO HII P- FUNK AKIWACHANA CLOUDS FM AELEZA JINSI MAREHEMU MAGWEA ALIVYOGEUZWA NG'OMBE WA MAZIWA

Kwa mara nyingine tena P-Funk amezungumzia sababu anazodhani zilipelekea marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa. Producer huyo ameichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama unyanyasaji kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya. “Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.” P funk Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records zikiwemo wa Ngwea, P-Funk amesema: “Niko kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote za Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm. Sababu kubwa ni uonevu wa haki miliki. Eti mnajiita number one radio station??. Mnajidaganya .Kisaikolojia wasanii wote mmewateka. Wote wanaona “bila kupeleka nyimbo zao Clouds hawatafanikiwa.”Mimi cha kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingine kwamba bila nyinyi tutaweza. Cha pili mnaingiza hela sana ya wadhamini lakini hamui-distribute kwa wanaohusika... "Mfumo wa kupeleka nyimbo Clouds nilianzisha mimi . Hivyo nitakua wa kwanza kujitoa na kuanzisha mfumo mwingine.””
Read More >>

DOWNLOAD SONG:MSWAKI - OPEN LETTER FOR MANGWEA


Kabla rapper Ngwea hajafariki, moja ya producer aliekuwa anafanya nae kazi ni producer, ambapo kazi hii ilikuwa ni kwa ajili ya Ngwea, na ilikuwa imebaki yeye tu kuja kuingiza verse zake kwababu chorus tayari ilikua ishaingizwa, lakini baada ya habari hizi mbaya kutufikia (kifo cha Ngwea), Mswaki ameamua kuingiza sauti yake mwenyewe na kutimiza kile alichokuwa anataka kukifanya Ngwea. ukisikiliza hii ngoma kama hujaambiwa kaimba nani, lazima utajua ni Ngwea kumbe ni Mswaki..R.I.P Ngwea
Read More >>

YANGA WAKABIDHIWA SHILINGI MILLIONI 25 ZA ZAWADI YA UBINGWA WA VODACOM NA KILIMANJARO

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe kushoto akimkabidhi mfano wa hundi Katibu Mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako leo katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha bia TBL iIlala
 
 










































 Kilimanjaro Premium Lager – wadhamini wakuu wa timu ya Yanga  imetoa kiasi cha shilingi milioni 25 kama zawadi kwa timu hiyo kwa kushinda Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013. 
Akikabidhi hundi ya Sh milioni 25 kwa Yanga SC, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema Kilimanjaro Premium Lager imefurahishwa sana na ushindi wa timu ya Yanga na kusema imejizatiti kikamilifu kuisaidia timu ambayo imeibuka bingwa katika ligi yenye ushindani mkubwa kutokana na kuibuka kwa timu mpya zenye nguvu.
“Yanga imekuwa ikicheza mpira mzuri kipindi chote cha msimu wa ligi kuu, na sio ajabu wao kuibuka washindi wa Ligi hii. Napenda kuwapongeza wachezaji wa Yanga, kocha na Uongozi mzima wa Yanga kwa  matokeo mazuri ya kushinda Ligi kuu kwa mara ya 24 sasa.”
 
Kavishe aliongeza kuwa zawadi hiyo ni sehemu ya sh bilioni 1.5 ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Yanga   na imetolewa kwa lengo la kuhamasisha klabu kujitahidi kwa ushindi zaidi na kusaidia klabu katika maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ambayo tayari Yanga ina sifa za kushiriki kutokana na ubingwa waliojipatia.
 
Akipokea hundi hiyo, Katibu mkuu wa Yanga , Bwana Lawrence Mwalusako alisema Yanga inaishukuru sana Kilimanjaro Premium Lager kwa mchango wao. Aliongeza kuwa Yanga ni timu nzuri na yenye nguvu kutokana na uongozi imara pamoja na udhamini mkubwa kwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.  
 
‘‘Mafanikio yetu ya uwanjani ni kielelezo cha mafanikio ya kampuni na pia (TBL) na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa ujumla ambayo imekuwa ikitusaidia sana. Kilimanjaro  Premium Lager imetoa mchango mkubwa sana katika kuipa timu msukumo uliopelekea mafanikio haya,’’ alisema Mwalusako.
 
Mwalusako aliongeza “Yanga sasa ina nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la kimataifa la soka kutokana na mafanikio haya’’.  “Tunaamini kuwa kutokana na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager tutaendelea kukua na kufanikiwa.’’
 
Yanga itawakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Kagam
Read More >>

Video: Wasanii walipokutana Leaders jana (May 29) kuchangisha fedha za msiba wa Albert Mangwea

Read More >>

Download New Audio: Kelly Rowland, Beyonce na Michelle Williams katika wimbo mpya ‘You’ve Changed’ (Snippet)


destinys_child

Ladies and Gentlemen warembo watatu walioweza kujichukulia umaarufu miaka ya nyuma kupitia brand ya Destiny’s Child, Kelly Rowland, Beyonce na Michelle Williams wamekutana tena katika “You’ve Changed”, lakini msiwe too excited sio kazi ya kundi!

Huu ni wimbo mpya wa Kelly Rowland ambaye ameamua kuwashirikisha group mates wake Beyonce pamoja na Michelle katika “You’ve changed me” itakayopatikana katika album yake ijayo “Talk A Good Game”.
Read More >>

JOSE MOURINHO ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE KUJIUNGA TENA NA CHELSEA

JOSE MOURINHO ni boss mpya wa Chelsea — na hiyo ni rasmi kwa mujibu wa gazeti la The Sun!

The Special One ameripotiwa kusaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya £40million jana usiku. 
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa juu wa Chelsea: “Ni rasmi Jose ni kocha wetu tena! Kila mtu anafurahia ujio wake - klabu, wachezaji na mashabiki. 
“Tayari tunajiaandaa na msimu ujao - tuna uhakika utakuwa msimu mzuri sana.” 

  
Mechi ya kwanza ya Mourinho inatarajiwa kuwa kwenye mechi ya mataarisho nchini Thailand dhidi ya  Singha All Stars XI, katika ziara ya huko Malaysia na Indonesia. 
Baada ya hapo The Blues wataenda Marekani kwenye michuano ya  International Champions Cup itakayohusisha timu za Real Madrid na Inter Milan, pia Everton, Juventus, AC Milan, Valencia na LA Galaxy. 
Read More >>

Msichana ajitokeza na kudai kuwa Justin Bieber ni baba wa mwanae mwenye miaka miwili!


justin-bieber1
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 27 amejitokeza na kudai kwamba staa mdogo mwenye matukio makubwa Justin Bieber alimpa ujauzito baada ya kufanya naye mapenzi tarehe 4 February 2010.

Chanzo kimoja kimeliambia jarida la Star kuwa msichana huyo alijifungua mtoto wa kike mwezi October 2010 baada ya kuwa na usiku wa pamoja na Bieber huko Miami Beach February 4, 2010 aliyekuwa akiperform siku hiyo.
Chanzo hicho kiliendelea kusema sababu za msichana huyo kutomwambia Bieber ambaye mwaka (2010) alikuwa na miaka 15, kuhusiana na mtoto huyo anayedai kuwa ni wake, ni kuwa alitaka kumlinda mwanae na familia yake kwa kutotaka kuwa kwenye spotlight.
Kwa mujibu wa jarida hilo, msichana huyo ambaye hajataka jina lake litajwe amesema anahitaji Justin Bieber ajue kuwa yeye ni baba wa mtoto wa kike wa miaka miwili, lakini hatahitaji pesa yoyote kutoka kwake na wala haitaji kuwa sehemu ya maisha ya ustaa wa baba wa mtoto wake.
Msichana huyo ambaye wakati anakutana na Bieber (kama anavyodai) alikuwa na miaka 25, aliongeza kuwa anamuachia maamuzi yote Justin Bieber mwenyewe kama atakuja kuhitaji kujihusisha kwa namna yoyote na mwanae baadae au laa.
Je wewe unaamini kuwa Bieber anaweza wa kuwa baba wa mtoto wa miaka miwili?
Read More >>

Wema: Sikuwahi kumsaliti Diamond na tulikuwa tunapendana sana

_DSC1063 copy
Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amefunguka kupitia jarida jipya la Mzuka kuwa katika uhusiano wake wote na Diamond hakuwahi kumsaliti.

Wema ambaye yupo kwenye cover la jarida hilo linalotolewa na kampuni ya Bongo5 Media Group, amefunguka kwa kusema kuwa yeye na Diamond walikuwa wakipendana sana.
wema2
“Maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema.
Wema amefunguka pia kuhusu jinsi Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.”
Katika jarida hilo ambalo linauzwa kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive.
Read More >>

(Video) Kidum Moves From Love To Party Songs. Are You Feeling His New Track ‘Enjoy’?

kidum
Kidum
When you mention the Kenya based Burundian artist ‘Kidum’ , Love comes to many people’s minds mainly because Kidum is known for his deep love songs. Kidum rocked the music scene with his love tunes and am talking about the likes of Mapenzi,Haturudi nyuma which he featured Juliana Kanyomozi, Nitafanya with Lady Jaydee and other hit-tracks that have set him aside as a great artist when it comes to singing about Love, relationships and matters of the heart.
Read More >>

HII NDO TASWIRA KUTOKA MSIBANI KWA MAMA MANGWAIR

Mama Mzazi wa msanii Albert Kenneth Mangwair, Bi Denisia Mangwair akiwa na simanzi msibani leo.Dada wa marehemu, Magreth Mangwair, naye akiwa na majonzi ya kuondokewa na kaka yake.
Ndugu na jamaa wakimfariji mama Mangwair.
NI simanzi na majonzi kutoka nyumbani kwa Mama Mzazi wa msanii Albert Kenneth Mangwair, Bi Denisia Mangwair (63) maeneo ya Kihonda ‘Mazimbu Road’ mkoani Morogoro ulipo msiba wa msanii huyo. Msibani hapo pia alikuwepo dada yake marehemu, Magreth Mangwair ambaye alikuwa na majonzi kwa kuondokewa na kaka yake mpendwa.
(PICHA ZOTE NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
Read More >>

SETH APAMBANA KUINUSURU KANUMBA THE GREAT FILM ISIFE


Seth Bosco.
 
 
 MDOGO wa aliyekuwa mwigizaji maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco amefunguka kuwa anafanya kazi kwa bidii ili kuinusuru Kampuni ya The Great Film aliyoiacha marehemu kaka yake isife.
 
 
Akichezesha taya na paparazi wetu, juzikati jijini Dar, Seth alisema kutokana na pengo kubwa aliloliacha Kanumba, anajaribu kufanya kazi kwa bidii za kuaandaa filamu mpya ambazo wanawashirikisha wasanii tofauti wa Bongo ili kuinusuru kampuni hiyo.
“Yaani nafanya kazi kwa bidii sana kwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni aliyoiacha Kanumba, japokuwa hatuwezi kufanya vizuri kama alivyokuwepo mwenyewe lakini tunaamini kujitahidi kwetu kutasaidia,” alisema Seth.
Read More >>

MAMA MZAZI WA ANDRE 3000 AFARIKI DUNIA

Mwakilishi wa mwanamuziki Andre 3000 amethibitisha kutokea kwa kifo cha mama yake mzazi Sharon Benjamin-Hodo, kutokana na Billboard.com
mama huyo alikutwa amekufa ndani ya nyumba yake iliyoko Atlanta siku ya jumatatu (May 27), siku ambayo ni siku ya kuzaliwa ya Andre 3000 akifikisha miaka 38.
mama yake na Andre alikuwa ni muanzilishi wa Starlight Camp kwa ajili ya watoto wasiojiweza, yenye kufanya kazi zake nje ya New Morning Light Missionary Baptist Church iliyoko Conley, Georgia.
Andre 3000 ni member wa kundi la OutKast.
Read More >>

MASKINI KUPA! SIKU CHACHE BAADA YA NDOA YAKE ALAZWA HOSPITALI KWA UGONJWA WA FIGO.SOMA STORI NZIMA HAPA

Na Imelda Mtema
MASKINI! Mwigizaji Idrissa Makupa ‘Kupa’ yuko katika wakati mgumu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Tabata General, jijini Dar baada ya kugundulika ana tatizo kwenye figo.
Mwigizaji Idrissa Makupa ‘Kupa’.
Akizungumza na paparazi wetu kwa tabu, Kupa alisema alianza kujisikia vibaya akapima malaria na vitu vingine havikuonekana ndipo alipofanyiwa uchunguzi zaidi na kugundulika kuwa ana tatizo kwenye figo.
 
Kupa akiwa hospitali.
“Nilipopimwa zaidi nimegundulika kwenye figo kuna mawe madogomadogo, mpaka sasa wanafanya utaratibu wa matibabu ili Mungu akijalia nipone,” alisema Kupa ambapo mkewe, Mary anayemuuguza naye akionesha kuguswa na tatizo hilo.
“Yaani hapa nilipo hata chakula hakipiti, naomba Mungu amjalie mume wangu apone haraka,” alisema Mary.
Wawili hao walifunga ndoa siku chache zilizopita.
Read More >>

ANGALIA PICHA ZA MWAKILISHI WETU KATIKA BBA ALIVYOJIACHIA BAFUNI NA DILISH.

Dillish na Nando wakioga
Jana (May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa romantic na kuonesha upendo (Romantic time). 
 Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzania Ammy Nando alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.
Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uruzi wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa kitanzania.
Dillish
Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi ya kushare na  Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. Jana Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold digger. Lakini second kadhaa baadae akafuta kauli yake na kumwambia kuwa alikuwa anatania. Really?!

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi kukumbwa na Eviction.
Read More >>

Vurugu zasababisha Bunge kuahirishwa hadi jioni.

Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha CUF kuwa ni chama cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni, wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...

Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge.. 

 
Kipengele kinachowasumbua katika hotuba ya Wenje ni hiki hapa...ambacho kimejaa facts na ukweli. Wakanushe hizi facts. Wajibu hoja si kumshambulia mtoa hoja. That is what argumentation is all about, let alone critical thinking.


Kitu gani si cha kweli hapa?


3.0. VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa ‘United Nations University’(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani kutoka nje katika mabadiliko ya kisiasa Tanzania ‘Donor Assistance and Political Reform in Tanzania’, inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka 1990-2010.


Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka nje ya nchi na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na taasisi kama Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo.


Pamoja na misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana duniani pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada hiyo.


Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado vyama vya siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya siasa katika mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina mbalimbali kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na mirengo ya kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo vyama vya siasa vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea kutoka nje ya nchi na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za uongo kuwa vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za magharibi.


Mheshimiwa Spika, CCM wao ‘wanajiita’ kuwa wapo mrengo wa kijamaa/kikomunisti na wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na nyenzo kutoka Umoja wa Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni ‘Socialist International’ kutoka katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP ,Uingereza kupitia chama cha Labour,China kupitia chama cha Kikomunist ,Marekani kupitia chama cha Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na kiufundi ambayo CCM imekuwa ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi hadharani hata mara moja kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea na hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.


Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(
www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.

Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.


Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.


Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .

Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.


Source:Jamii Forums
Read More >>

Upelelezi vurugu za Lema Uhasibu wakamilika


MBUNGE wa Jimbo la Arusha Godbless Lema (aliyevaa kombati nyeusi) anatarajiwa kusomewa maelezo ya awali Julai 2 mwaka huu baada ya upelelezi wa kesi yake kukamilika. Lema anakabiliwa na kesi ya uchochezi, kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani katika Chuo cha Uhasibu Njiro, Arusha. Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Eliainenyi Njiro aliiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Msofe, Njiro aliiomba Mahakama hiyo kupanga tarehe ya kusoma maelezo ya awali ya mtuhumiwa.

Naye Wakili Humphrey Mtui anayemwakilisha Lema aliiomba Mahakama kupanga muda wa mbele baada ya Juni 28, Mwaka huu ili mteja wake amalize vikao vya Bunge mjini Dodoma.

Kutokana na mapendekezo hayo Hakimu Mkazi Msofe alikubaliana na maombi hayo na kupanga shauri huilo hadi Julai 2 mwaka huu.

Mtuhumiwa Lema anadaiwa kati ya Aprili 24, Mwaka huu kutenda kufanya uchochezi,kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani kinyume na kifungu cha 390 na kifungu cha 35 cha Sheria ya makosa ya jinai sura namba 16, marejeo ya 2002.

Akiwa katika Chuo cha Uhasibu (IAA) Aprili 24, mwaka huu, Lema anadaiwa kutamka maneno yaliyosababisha uvunjifu wa amani.

Maneno yanayodaiwa kutamkwa na Mbunge huyo ni “Mkuu wa Mkoa anakuja kama anakwenda kwenye send off na hajui mahali chuo hicho kilipo na alishindwa kuwapa pole wanafunzi hao kwa kufiwa na mwanafunzi mwenzenu.

Mengine ni “Mkuu huyo hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu pamoja na kuwa hakuwasaidia kutokana na matatizo yao.”

MTANZANIA
Read More >>

TAARIFA KUHUSU MSIBA WA MANGWEHA KUTOKA KWA BABA MDOGO

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko
 Mbamba Bay kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake 
mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha 
ambaye naye yuko Mbamba Bay kuwa watu watakutanika Mbezi
 kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam
 Mbezi Beach. Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika
 lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika 
Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam 
pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. Kuhusu
 mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo 
amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika 
hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya 
taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni
 jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho 
baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha
 familia watatoa taarifa.
Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...