Makamo
wa rais mpya wa Kenya, William Ruto, ameiomba mahakama ya kimataifa ya
uhalifu ICC iahirishe kesi yake inayodai kuwa alishiriki katika
uchochezi wa mapigano yaliyofuata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Kesi
hiyo imepangwa kuanza mwezi wa May huko The Hague lakini mawakili wa
Bwana Ruto wanataka iakhirishwe hadi mwezi Novemba wakisema kuwa
wanahitaji muda zaidi
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa huenda huu ni mpango wa kutaka kesi hiyo icheleweshwe.
Katika machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 watu zaidi ya 1,000 waliuawa.