KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa jimbo la arusha mjini
Godbless lema ameingia Kitanzini huku akihusishwa na Vurugu za Chuo
cha uhasibu Arusha ambapo chuo hicho kwa sasa kimefungwa mara baada ya
Vurugu kubwa kuibuka chuoni hapo kwa madai uongozi wa chuo haufuatilii
suala la mauji ya wanafunzi wa chuo hicho.
Akiongea na Vyombo vya habari mapema leo mkuu wa mkoa wa Arusha
Magesa Mulongo alisema kuwa Mbunge Lema amesababisha vurugu ambazo
zililazimu Jeshila polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya
wanafunzi ambao walitaka kuandamana mara baada ya mwanafunzi mwenzao
Hendry Kagu (22)kuuwawa na watu wasiojulikana Juzi.
Magesa alisema kuwa Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilidai kuwa
Mwnaafuzni huyo alichomwa kisu eneo la shingoni lakini wanafunzi
walikusanyika kwa madai ya kujadili juu ya kifo hicho na ndipo Lema
alipofika na kuaanza kushawishi juu ya wasiwasi wa Kifo hicho.
Aidha ilidaiwa kuwa mara baada ya ushawishi huo ambao pia ulikuwa
unadai kuwa mkuu wa chuo anatakiwa kukamatwa ndipo vurugu kubwa sana
zilipoibuka ambapo wanafunzi hao walitumia ushawishi wa Lema na kutaka
maandamano hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa huku pia wakipanga kudhuru
madereva wa Boda boda ambao wangekutana nao.
“Lema alipowashawishi wanafunzi hao wakamkate mkuu wa chuo na pia
wafanye maandamano basi yeye mwenyewe alipiga simu kwa viongozi wa
Serikali hapa Mkoani na kudai kuwa hali imechafuka sana huku Uasibu
lakini kwa kuwa alikuwa ameshapachika roho ya fujo wanafunzi
waliendeleza fujo hizo ambapo tulilazimkika kufika lakini hatukuweza
kuvumilia hali hiyo ya vurugu’alisisitiza Magesa.
Pia aliendelea kwa kusema kuwa alipofika katika eneo lka Tukio akiwa
kama Mwakilishi wa Raisi mkoa wa Arusha lakini bado wanafunzi hao
hawakutaka kumsikiliza huku wengine wakiendelea kutoa maneno ya kejeli
na kuzomea kuwa hawezi kuwasaidia kitu chochote kile
Kutokana na hali hiyo Alidai kuwa Jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati ambapo walitumia mabomu ya machozi kuwatanya maelfu ya wanafunzi ili kurudisha amani kwa muda ndani ya chuo hicho cha uasibu lakini hali haikuwa hivyo.
Kutokana na hali hiyo Alidai kuwa Jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati ambapo walitumia mabomu ya machozi kuwatanya maelfu ya wanafunzi ili kurudisha amani kwa muda ndani ya chuo hicho cha uasibu lakini hali haikuwa hivyo.
“nimeshangazwa sana na hii hali ambayo imetokea kamwe wanasiasa kama
Lema hawapaswi kuingilia masuala ya Vyuo kwa kuwa kamwe siasa haiwezi
kuendana na vyuo lakini kama mbunge anapovuruga amani je nani wa
kujenga na kuimarisha amani ya Jiji kama Lema angekuwa anataka
kuwasaidia angeingia kwenye uongozi na wala sio kwenda kwa wanafunzi
‘alibainisha Magesa.
Kutokana na hali hiyo Magesa alisema kuwa kwa sasa Lema anatafutwa na
Jeshi la Polisi lakini pia mpaka sasa baadhi ya Vinara ambao
walisababisha vurugu hizo kwa madai kuwa wanamtetea mwenzao Marehemu
Hendry wanashikiliwa na Polisi kwa mahijiano zaidi huku chuo hicho
kikiwa kimefungwa kwa muda usiojulikana chini ya Wizara ya Fedha.
Awali akiongelea tukio hilo Naibu Mkuu wa Chuo hicho cha Uasibu
Faraji Kassidi alisema kuwa wamelazimika kufunga chuo hicho ili waweze
kutuliza fujo ambayo ingezaa vifo vingi zaidi hivyo kila mwanafunzi
anatakiwa kuondoka katika chuo hicho ndani ya masaaa kadhaa.
Faraji alisema kuwa kwa mamlaka aliyopewa anatakiwa kufunga chuo hicho
kwa muda usiojulikana ambapo pia uchunguzi wa kifo cha marehemu Hendry
bado kinachunguzwa na vyombo vya usalama.