Wateja waBenki ya NMB wakipata maelekezo ya huduma za JISEVIE kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la NMB House Edith Mavura. Huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile, huduma inayomuwezesha mteja kupat a huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB
Wateja
wa Benkiya NMB wakipata maelekezo yanayohusu maboresho ya huduma
ijulikanayo kama JISEVIE kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la Bank House,
Salvatory Mushi .Jisevie inamsaidia mteja wa NMB kupata huduma za
kibenki sehemu yoyote atakapokua bila kufika kwenye tawi la NMB.Mteja
ataweza kutumia simu yake ya kiganjani na kutembelea Mashine za kutoa
fedha ili Kujisevia.
Ofisa wa
NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi akimwelekeza mteja wa NMB jinsi
ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa
NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata
huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB
Ofisa wa
NMB tawi la Loliondo, Lembris Lesion akimwelekeza Mchungaji mstaafu,
Ambelikile Mwaisapile jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA
huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile
.Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila
kufika kwenye tawi la NMB.
Na Mwandishi Wetu
NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.
Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelemisha wateja wake aina mbalimbali ya huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia kampeni yake maalum iitwayo JISEVIE.
Na Mwandishi Wetu
NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.
Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelemisha wateja wake aina mbalimbali ya huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia kampeni yake maalum iitwayo JISEVIE.
Huduma
zilizojumuishwa katika mpango huu maalum wa Jisevie ni pamoja na Huduma
ya NMB mobile, Huduma ya NMB PesaFasta, Huduma ya NMB ATM na huduma ya
kuweka na kutoa fedha kupitia Vodacom Mpesa.
“ Mpango
huu wa kuelemisha wateja juu ya huduma mbali mbali wanazoweza kuzipata
bila ya kupitia benki, yaani Jisevie unalenga katika kuendelea kutoa
huduma bora zaidi , kuvutia na za haraka zaidi wakati wowote mteja
anapohitaji huduma za kibenki”, alisema bwana Arjan Molenkamp, Afisa
Mkuu wa Biashara ya Wateja Binafsi.
Wateja
ambao wataweza kutumia moja ya huduma hizi zilizoainishwa katika mpango
huu wa Jisevie watapata faida mbalimbali ikiwemo; kutokutumia fedha
taslimu kulipia huduma mbali mbali, kuweka au kutoa fedha mahali popote
kwa kutumia huduma ya Vodacom Mpesa, Kutuma fedha kwa mtu yeyote asiye
na akaunti wala kadi ya ATM ya NMB kwa kutumia NMB PesaFasta na
kutohitaji kutembelea tawi lolote la benki ya NMB ili kuweka fedha
kwenye akaunti yako.
Wateja wa
NMB sasa wanaweza kupata huduma za kibenki popote walipo bila
kutembelea tawi la NMB. Haya yote yametokana NMB Jisavie ambayo
itamwezesha mteja wa NMB kuwa na NMB Mobile,NMB Pesa Fasta ,POS,NMB
ATM,Huduma ya kuweka na kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda
M-Pesa na M-Pesa kwenda Akaunti ya NMB,Zaidi ya hayo yote NMB inalenga
kumuwezesha Mteja wake aweze kujihudumia mwenyewe bila kufika kwenye
tawi la NMB.
Faida
nyingine anazoweza kupata Mteja wa NMB kwa kupitia mpango huu wa Jisevie
ni pamoja na kuangalia salio la akaunti yako, kupata taarifa fupi ya
matumizi ya akaunti yako, kununua Luku,Kulipa ankra ya Maji-DAWASCO,
kulipia bili ya King’amuzi ya DStv, Kulipia kodi za Mapato na kununua
muda wa hewani.




