Mkuu wa
kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin
Twissa(katikati)akiongea na Mshindi wa Droo ya mwishi ya "MAHELA
"Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia shilingi
Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini
Bw.Mrisho Milau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom
Tanzania,Bw. Benjamin Michael.
Kutoka
kushoto,Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho
Milau,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu,pamoja na
Meneja wa Huduma za ziada wa kampuni hiyo, Bw. Benjamin
Michael,wakichezesha droo ya mwisho ya "MAHELA"ambapo Bw.Valelian
Nickodemus(22)Mwanafunzi wa Chuo cha uwalimu Mkoani Kigoma alijishindia
kitita cha shilingi Milioni 100,kupitia promosheni hiyo.
Mkuu wa
kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin
Twissa(katikati)akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara
baada ya kumpata mshindi wa Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian
Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia shilingi Milioni
100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Mlau
na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin
Michael.
Hatimaye
Mshindi wa Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela amepatikana
ikishuhudia Mwanafunzi chuo cha Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian
Nickodemus(22) akiibuka mshindi kupitia droo kubwa iliyochezeshwa leo
jumatatu.
Mshindi
huyo amepatikana miongoni mwa mamilioni ya washiriki walioshiriki
kucheza katika promosheni hiyo, Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia
ya simu Mshindi huyo ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kumuwezesha
kushinda kiasi hiko kwani hayakuwa mategemeo yake katika maisha yake.
"Watu
wengi hawakuwa wanaamini kuwa Promosheni hizi ni za kweli, Sikuwa na
pesa ya kucheza moja kwa moja katika Promosheni hii ila nilipotumiwa
pesa ya matumizi na mzee niliamua kuweka na kushiriki katika Promosheni
hii, Hakika nimefurahi sana na ninawashukuru Vodacom, alisema
Nickodemus.
Kwa
upande wake mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twissa amewapongeza Wateja wa mtandao huo kwa kushiriki
katika promosheni hiyo na kumpongeza kwa upekee mshindi wa Promosheni
hiyo na kujinasibu kuwa anajivunia mafanikio ambayo Promosheni hiyo
imeyapata kwa kufanikiwa kubadili maisha ya mamia ya Watanzania.
"Sisi
kama Vodacom tumefurahi kwa kumpata mshindi wetu wa mwisho ambaye
ameibuka kidedea kati ya Mamilioni ya Watanzania lazima tukiri kuwa ni
bahati kubwa na tunatoa pongezi za kipekee kwa mshindi wetu, alisema
Twissa na kuongeza kuwa "Zaidi ya yote tunajivunia kwa upekee kabisa
namna ambavyo promosheni hii imebadilisha mamia ya maisha ya Watanzania,
Tumepata washindi kutoka katika Nyanja mbalimbali wakiwemo wakulima,
wafanya biashara ndogondogo wanafunzi pamoja na wastaafu wengi ambao nao
wameendelea kuboresha maisha yao.
Tangu
Promosheni ya MAHELA kuzinduliwa tarehe 24 Mwezi wa kwanza na washindi
333 wamepatikana na kushuhudia kiasi cha Shilingi milioni 480 zikitolewa
hadi sasa.



