MKE
wa mtu ambaye jina lake halikufahamika mara moja (pichani),hivi
karibuni yalimkuta makubwa baada ya kuibiwa vitu vyake vyote vilivyokuwa
ndani ya pochi na dereva wa Bajaj ambaye pia jina lake halikufahamika.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo dada huyo alikodi Bajaj hiyo toka nyumbani kwake,
Kinondoni-Shamba jijini Dar kwenda kujirusha katika klabu moja ya usiku
iliyopo Mwananyamala ndipo alipolizwa pochi hiyo iliyokuwa na fedha
(zaidi ya elfu hamsini) pamoja na vitambulisho.
Chanzo
hicho kilizidi kueleza kuwa, kabla hajafika klabu, dada huyo aliamua
kumpitia shosti yake aliyekuwa katika Baa ya Uhuru Peak, Mwananyamala
ili wakajirushe pamoja ndipo dereva huyo alipomfanyizia.
“Alipofika
hapa Uhuru Peak akaacha pochi yake ndani ya Bajaj ili amshtue fasta
rafiki yake ndipo dereva alipotumia mwanya huo kutokomea
kusikojulikana,” kilisema chanzo hicho.
Baada
ya dakika kadhaa, dada huyo alitoka nje na kuanza kuangaza huku na
huko ghafla akapata msala mwingine wa kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi
lililokuwa katika msako wa kuwakamata machangudoa.