
Maharusi Alex Kusaga na Mkewe Evelyn wakilisha keki ya upendo usiku huu
ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Serena jijini dar.


Ulifika wakati wa kufungua shampeni.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho,Lina,Barnaba na
Amin wakitumbuiza usiku huu kwa pamoja kwenye mnuso wa mdau Alex Kusaga kutoka
mjengoni,Clouds Media Group.



Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mnuso huo wa
nguvu.

Bibi harusi,Evelyne Julla akitoa tabasamu la nguvu na lenye
furaha mara baada ya kuikamilisha ndoto yake ya kumpta mwenza wake wa
maisha,Bwa.Alex Kusaga wa Clouds Media Group.

Maharusi wakizifurahia pete zao za ndoa mara baada ya mapumziko
mafupi kabla ya kuingia mnusoni jioni ya leo ndani ya hotel ya Serena jijini
dar.

Wakishoo love na mdogo wake Alex Kusaga,ambaye ni wifi ya bibi
harusi.

Maharusi wakionesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga
harusi ndani ya kanisa la St.Immaculata,Upanga jijini Dar.

Maharusi wakila kiapo cha ndoa
