


Redsun


Ili kupata picha halisi ya jinsi concert hiyo ilivyokuwa kubwa na yenye mafanikio, tumemtafuta mtangazaji maarufu wa Kenya Mzazi Willy M. Tuva anayetangaza kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen na Mseto East Africa cha Citizen TV aliyekuwa shuhuda kwenye viwanja hivyo kutuelezea. Na hivi ndivyo alivyosimulia:
“Chameleone ni msanii mkubwa sana Afrika Mashariki na waganda wanamkubali sana. I observed a number of things ambazo Ningependa watu wajue. Chameleone amejipanga vilivyo kwenye maandalizi ya show na performance. Alitawala jukwaa kwa masaa mengi bila kuchosha watu. Aliimba na band.


Jose Chameleone na mwanae



Mke wa Chameleone (Daniella) kulia akiwa na shoga zake kumshuhudia mumewe akifanya yake

Redsun na Profesa Jay wakimshuhudia Dokta


Mzazi
Tuva kwenye Twitter aliandika: A mzungu from Norway on stage singing
@JChameleone’s #Valuvalu at the #Badilisha concert. Celebrating East
African Music

Chameleone alikuwa na umati mkubwa sana.Kikubwa ni kuwa lugha ya Kiswahili inafaa itukuzwe. Msanii anayeimba Kiswahili anakubalika zaidi kuliko anayeiga tamaduni za Magharibi. Chameleone ni mfano mzuri. Anakubalika kwao na amepenya Kenya na Tanzania. Kwanini? Sababu anaunganisha Uganda na Afrika Mashariki.








Jiulize mbona Bobby Wine na Bebe Cool hawajapenya zaidi nje ya Uganda? Jibu unalo.. Niliwauliza baadhi ya watu wakasema hata kama hawaelewi vizuri (Kiswahili) wanapenda muziki wake na melody zake. Pia anawafanya waganda waelewe Kiswahili. Badilisha ndio wimbo mkubwa zaidi Uganda.”











Baada ya show hiyo Chameleone ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook:
“Thank you for making this a remarkable date on my music career calendar. we made history as a team! Badilisha live 26th April 2013…….2014 here I come! Leone Island tugende tukole!