
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka
kuwa hakuna kinachoweza kumtenganisha na msanii wa muziki wa kizazi
kipya, Elius Barnabas ‘Barnaba’ kwani walikotoka ni mbali.
Shilole na Barnaba hivi karibuni walinaswa maeneo ya Coco Beach wakila
bata lakini baada ya kuwaona mapaparazi wakizunguka kutafuta matukio,
Barnaba alitimua mbio na kumuacha Shilole ambaye bila hiyana
alitiririka:
“Jamani
mimi na Barnaba hakuna cha kututenganisha japokuwa watu wanachonga sana
hata kuandikwa kwenye magazeti lakini bado tunaendelea tu, hivyo najua
hakuna mtu anayeweza kututenganisha.”



