- Waliotajwa katika orodha hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Pia wamo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Dk Hussein Mwinyi na wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo.
Dar es Salaam. Ikiwa imebaki
miaka miwili kufanyika ka uchaguzi mkuu nchini, Kamati ya Vijana wapenda
Amani Tanzania, imetaja majina ya watu wanne wenye sifa za kuwania
urais nchini, huku ikieleza kuwa uzoefu wa miaka mingi si kipimo kizuri
cha uongozi bora.
Kamati hiyo imesema Watanzania wanatakiwa
kuwaogopa watu wanaojitaja wazi kuutaka urais, huku wakitumia majukwaa
ya kisiasa, kidini, kijamii, kiutamaduni na michezo kutoa misaada
mbalimbali kwa maelezo kuwa watu hao wakipewa nchi, wataongoza kwa
maslahi ya kundi fulani.
Waliotajwa katika orodha hiyo ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa
Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk Hussein Mwinyi na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,
January Makamba.
Katika orodha hiyo, kamati hiyo haikuwataja
viongozi waliowahi kujitangaza kutaka nafasi hiyo na ambao
hawajajitangaza, lakini wanaonekana kuwa na dhamira ya kugombea urais
mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Chifu Msopa, alisema wakati umefika kujadili
mahitaji ya nchi kiuongozi kwa manufaa ya siku zijazo,.
Katika maelezo yake, Msopa alitaja sifa za kila
kiongozi aliyemtaja katika orodha hiyo na kwamba kama ikitokea watu hao
wakashindwa kusimamishwa na vyama vyao kuwania urais mwaka 2015,
kamati hiyo itamuunga mkono yeyote ambaye atakuwa na sifa zinazofanana
na watu hao wanne.
Sifa za waliotajwa
Kwa upande wa ZittoMsopa alisema ana uwezo mkubwa
kiungozi, na kwamba mfano ni wa jinsi anavyosimamia Kamati ya Bunge ya
Mashirika ya Umma na kufichua madudu.
Kwa upande wa Mbatia, alisema kiongozi huyo ni
mzalendo wa nchi yake, ametulia na ana hekima kubwa ya kiuongozi na
kwamba busara zake zimedhihirika kwa jinsi anavyoongoza Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD) kama mwenyekiti.
“Amekuwa akipigania ubora wa elimu ya watoto wetu
na kujali ujenzi wa taifa bora zaidi na ana uwezo wa kufanya kazi na
viongozi kutoka vyama vyote vya siasa.
Akitaja sifa za Makamba alisema wakati akiwa
mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini alikuwa msema kweli, jasiri
kwa kuikosoa Serikali inayoongozwa na chama chake.
Alisema Makamba wakati akiwa Wizara ya Mambo ya Nje, alikuwa
msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka mitano na kufafanua kuwa hiyo
ni sifa ya muhimu kwa kiongozi.
Akimzungumzia Dk Mwinyi, Msopa alisema ana busara
na ndio sababu ya kuongoza vizuri wizara nyeti ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi