Winnie
Mandela amebainisha maumivu makali anayohisi kumwona mumewe wa zamani
Nelson anateseka hospitalini, akisema ataendelea kumpenda wakati wote
licha ya kuachana kwao.
Pia
alisema kwamba anafurahia uhusiano wa karibu na mke wa pili wa mpinga
ubaguzi wa rangi huyo, Graca, na kutania kwamba wanamchukulia kama 'mume
wetu'.
Wanawake
hao wawili wamekuwa kando ya kitanda cha Mandela kwa wiki nne zilizopita
huku akiendelea kutibiwa maambukizi katika mapafu kwenye hospitali moja
mjini Pretoria.
Winnie aliachana na rais huyo wa zamani mwaka 1996, lakini wawili hao wameendelea kuwa karibu kufuatia familia yao pana.
Alipoulizwa
kama bado anampenda, alisema: "Nitampenda milele, ni baba wa watoto
wangu... Hakuna kilichobadilika sababu alifunga ndoa na mtu mwingine.
"Hakuna mama anayeweza kusema wanawachukia wapenzi wao bila kujali tukio gani la kijamii lililo kati yao."
Pia alisisitiza kwamba anaelewana vema na Graca, ambaye aliolewa na Mandela mwaka 1998.
"Namwita
mdogo wangu na ananiita dada yake mkubwa, tunashirikiana kila kitu,"
alisema Winnie. "Anapoongea na mimi, anazungumzia kuhusu 'mume wetu".
"Ni familia moja, wote tuko kwenye hali moja kiroho."
Mwanasiasa
huyo moto alikanusha vikali ripoti kwamba ndugu wa Mandela wamekuwa
wakilumbana kumuweka au kutomuweka kwenye mashine ya kupumulia.
"Ilikuwa ni upuuzi kushauri kwamba tunahitaji kufanya uamuzi kuondoa mipira hiyo," alisema Winnie.
"Unaposikia waumini wakisema wanaiombea familia kutochomoa mipira hiyo, nafikiri kwamba hilo limefika mbali kidogo."
Binti
yake Zindzi aliongeza: "Watu wanaposema, "Familia hiyo lazima isalimu
amri" - kusalimu amri kwa kipi? Ni kati yake na muumba wake, haituhusu
kwa namna yeyote ile."
Winnie
pia alikuwa na maneno makali kwa Rais Jacob Zuma na chama tawala cha ANC
kwa kupiga picha na Mandela anayeteseka mwezi Aprili.
Mzee
Mandela mwenye miaka 94 alipigwa picha akiwa mwenye afya tete, akiwa
amezungukwa na Zuma na maofisa wengine, na Winnie alisema kwamba picha
hiyo ilithibitisha kuwakera ndugu.
Barack
Obama alilazimika kufuta mkutano aliopangiwa kukutana na kiongozi huyo
wakati wa ziara yake Afrika Kusini ambayo ilihitishwa juzi.