Hamida
Hassan 25 Mke wa Marehemu akiwa amejiinamia kwa hudhuni kutokana na
Mwanaume aliyekuwa ametengana naye kufa kwa kujinyonga kutokana na wivu
wa kimapenzi uliosababishwa na kuishi nyumba zao zikiwa zinatazamana
mtaa wa njedengwa Manispaa ya Dodoma.(Picha na John Banda)
Balozi
katika mtaa wa Njedengwa, Sikitu Mrisho akiwafafanulia jambo waandishi
wa habari baada ya marehemu mwenye majina zaidi ya manne ya
Paulo,Yakobo, Hassan na Joti kukutwa amekufa kwa kujinyonga kwenye
nyumba aliyokuwa akiishi Njedengwa manispaa ya Dodoma
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Balozi katika mtaa wa Njedengwa Sikitu Mrisho akiendelea kufafanua jambo
Na John Banda, Dodoma
MWILI wa Mmoja
mmoja aliyekuwa akitumia zaidi ya majina manne umekutwa ukinin’ginia kwenye paa
la nyumba aliyokuwa akiishi iliyopo katika kitongoji cha Njedengwa, kata ya
Dodoma makulu baada ya kudaiwa kujinyonga.
Mwili huo
ulikutwa ukiwa umehalibika vibaya kutokana na kuvimba baada ya kuchelewa
kugundulika.
Balozi wa
mtaa huo Sikitu Mrisho aliliambia Jambo leo kuwa watoto waliokuwa wakicheza nje
ya nyumba hiyo ndiyo waliomzindua na yeye kuamua kufuatilia.
Sikitu alisema
kuwa baada ya kufuatilia akabaini ukali
wa ile harufu na alipofunua pazia lililokuwa limeufunika mlango akagundua
ulikuwa umefungwa kwa ndani na ile harufu iliongezeka ndipo akaamua kuita
majirani na kuuvunja mlango huo kabla ya kuita polisi.
Alisema walipoingia
waliukuta mwili wa marehemu huyo mwenye utatanishi wa jina lake kutokana na
kutumia majina manne tofauti ya Paulo, Yakobo, Mohamed na Hassan Joti ukiwa
tayali umeanza kupasuka.
‘’Mwanangu
pamoja na chupa hizo zilizosagwa malangoni bado huyu baba akaamua kujitundika,
lakini kulikuwa na ugomvi kati yake na mkewe anayeishi hiyo nyumba unayoiona
hapo baada ya kutengana na mwanamke akawa na wanaume wengine pengine ndiyo
sababu ya kujinyonga’’, alidokeza Balozi huyo
Kwa upande
wake Mke wa Marehemu huyo Hamida Hassan [25] mkazi wa njedengwa alikiri kuwa na
ugomvi na Mume wake kutokana na yeye kuwa mfanyabiashara ya pombe za kienyeji
ambazo mumewe hakutaka kutokana na biashara hiyo kukosa heshima.
‘’Aliwawahi
kuniambia nisiende kufanya biashara hiyo eti kwa sababu nikiwa kirabuni wanaume
wengi wananishikashika hivyo tukawa tunagombana na tulipofika kwa mwekiti wa
mtaa tukaambiwa kwanza kila mtu aishi peke yake’’, alisema mwanamama huyo
Aidha
alisema yeye hakuwahi kujua jina lake halisi kutokana na kutumia majina hayo
manne na pia hakuwahi kujua nyumbani kwa wakweni wapi pamoja nay eye kumpeleka
kwao lakini alipomtaka ampeleke kwa wazazi wake alikataa na kumwambia ni Mgeta
wakati siku nyingine alimwambia ni kihonda mkoani morogoro.
Kamanda wa
Polisi David Misime alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka watu
wasikimbilie kujinyonga wakati wa matatizo badala yake watafute usuruhisho wa matatizo yao kwa
kuwashirikisha watu wengine wakaribu ili wapate kushauriwa.