Ghasia zimekuwa jambo la kila mara Misri tangu Morsi kuondolewa mamlakani
Watu
saba wameuawa mjini Cairo usiku wa kuamkia leo kufuatia makabiliano
makali kati ta wanajeshi wa serikali na wafuasi wa rais wa Misri
aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi.
Polisi
walitumia vitoa machozi kuwatawanya na kuwasukuma nyuma waandamanaji
hao ambao walikuwa wakiwarushia mawe huku wakiwa wamefunga barabara kuu
inayoelekea kati kati mwa mji mkuu.
Ghasia hizo zimetokea huku naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, William Burns akiwa ziarani nchini humo.
Waziri huyo amesema taifa hilo limepewa nafasi ya pili kurejesha utawala wa kidemokrasia.
Bwana
Burn alifanya mashauriano na viongozi wa serikali ya mpito ya nchi
hiyo, lakini viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood, walisusia mkutano
huo.
Awali
mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi
wamepambana na vikosi vya usalama katikati mwa mji wa Cairo na
kuwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa machozi.
Mapigano
hayo yanajiri muda mfupi baada ya mjumbe mkuu wa Marekani William Burns
kutoa wito kwa vikosi vya usalama kujizuia kwa kiwango kikubwa katika
kukabiliana na maandamano hayo.
Makabiliano
yalifanyika baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayezuru
Misri, kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa wanajitahidi
kutuliza ghasia wakati wakijizuia kufanya mauaji yoyote.
Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi.
Lakini chama cha Muslim Brotherhood kimesema haikina nia ya kukutana na waziri huyo.
Akizungumza
baada ya kukutana na viongozi wa serikali mpya inayoungwa mkono na
jeshi nchini, mjumbe huyo, William Burns, amesema Misri imepewa nafasi
ya pili kufuatia kupinduliwa na jeshi Mohammed Morsi.
Alikutana
na serikali inayoungwa mkono na jeshi nchini lakini Muslim Brotherhood,
inasema haina mpango wa kukutana naye. Naibu rais wa tawi la kisiasa la
chama cha Morsi, Muslim Brotherhood,Essam el-Erian, ametoa wito wa
utulivu.BBC SWAHILI