Sehemu ya waandamanaji wakiwa wamekusanyika mitaani mjini Cairo. |
Idadi ya
mashambulio ya udhalilishaji na ubakaji dhidi ya waandamanaji wanawake
kwenye Uwanja wa Tahrir nchini Misri imefikia 91 katika siku nne tu.
Makundi
ya uhalifu yaliwashambulia wanawake hao huku mamilioni ya waandamanaji
yalivamia mitaani kushinikiza Rais Mohammed Morsi kuachia ngazi.
Jana
jeshi la Misri lilisonga mbele kuimarisha umiliki wake kwenye taasisi
nyeti, hata kufikia kuweka maofisa wake kwenye chumba cha habari cha
televisheni ya taifa - muda wa mwisho walioweka viongozi wa jeshi kwa
Rais Morsi kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Misri au vinginevyo jeshi
lingeweka mipango yake yenyewe ya kisiasa mchana huo wa jana.
Shirika
la Haki za Binadamu liliripoti kwamba Oparesheni ya Kuzuia Vitendo vya
Udhalilishaji wa Kijinsia inasemekana wanawake wanne kati ya walihitaji
msaada wa matibabu, wakiwamo wawili ambao waliokolewa kwa gari la
wagonjwa.
Mwanamke
mmoja alihitajika kufanyiwa upasuaji baada ya kubakwa kwa kutumia 'kitu
chenyr ncha kali' kwa mujibu wa kundi la haki za wanawake la Nazra for
Feminist Studies.
Wanawake walipigwa kwa minyororo ya chuma, fimbo na viti, na
kushambuliwa kwa visu - baadhi ya mashambulio yalidumu kwa dakika 45
kabla ya kufanikiwa kutoroka.
Wiki iliyopita, mwandishi wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22
alibakwa na kundi la wahuni kwenye Uwanja huo wa Tahrir na alilazimika
kufanyiwa upasuaji kufuatia majeraha yake makubwa - shambulio lake la
kutisha la ubakaji ni kumbukumbu ya vurugu za Uwanja wa Tahrir mwaka
2011 wakati mwakilishi wa shirika la habari la CBS Lara Logan alipopigwa
na kudhalilishwa kijinsia na kundi imara la wanaume 200.
"Mashambulio hayo ya maandamano ya Uwanja wa Tahrir yanaonesha
kushindwa kwa serikali na vyama vyote vya siasa kukabiliana na ghasia
ambazo wanawake wa Misri wanakabiliwa nazo katika maisha ya kila siku
kwenye maeneo ya wazi," alisema Joe Stork, mkurugenzi msaidizi wa
Shirika la Haki za Binadamu huko Mashariki ya Kati.
Morsi alitarajiwa ama kujiuzulu au kulazimishwa kuachia madaraka na
jeshi jana, lilidai shirika la habari la nchini hu,o, huku picha
zilizopatikana zikionesha waandamanaji wakijaribu kutungua helikopta ya
kijeshi.
Ghasia kati ya waandamanaji wanaompinga Morsi na makundi ya upinzani
ziliongezeka usiku wa kuamkia jana kwa matatizo katika mji mkuu wa Cairo
ikishuhudiwa takribani watu 23 wakipoteza maisha na 200 wakijeruhiwa.
Takribani watu 39 wameuawa kwenye mapigano tangu Jumapili iliyopita,
na kuibua hofu mgogoro huo unaweza kulipuka na kuzusha mauaji makubwa.
Mapigano hayo yamekuja saa kadhaa baada ya viongozi wa jeshi la nchi
hiyo kuweka muda wa mwisho kwa Rais Morsi kutafuta suluhu ya mgogoro wa
kisiasa nchini Misri au vinginevyo jeshi hilo litaanzisha mpango wake wa
kisiasa.
Jeshi limepanga kumng'oa Morsi endapo hakutafikiwa muafaka wowote, kusimamisha katiba, kuvunja bunge na kuweka uongozi mpya.
Rais Mohammed Morsi ambaye jana alipuuza agizo la jeshi kulazimisha
kufikiwa muafaka wa mgogoro wa kisiasa nchini Misri, alitoa hotuba ya
kusisimua iliyorushwa moja kwa moja kwa taifa hilo.
Morsi,
ambaye mwaka mmoja uliopita alitawazwa kama Rais wa kwanza huru wa
kuchaguliwa nchini Misri, aliapa kulinda 'kuhalalishwa kwake kikatiba'
kwa maisha yake yote.