Na Khadija khamis –Maelezo Zanzibar
NAIBU
wazri wa kilimo na mali ya asili Mtumwa Kheri Mbarouk amewataka
wakulima wa mboga mboga na matunda kuitumia fursa wanayoipata kupitia
taasisi ya kusaidia wakulima wa mboga mboga na matunda Tanzania (TAHA)
katika kukiimarisha kilimo hicho.
Aliyaeleza
hayo jana waziri huyo katika uzinduzi wa ofisi na miradi ya TAHA
Zanzibar iliyofanyika katika ofisi ya mfuko wa barabara Kikwajuni mjini
Zanzibar.
Alisema
ipo haja kwa wakulima hao kuimarisha kilimo hicho, kukitunza na
kuithamini ili iwe mkombozi katika kuleta mapinduzi ya kilimo.
“Mafanikio
tuliyoyapata yameleta tija na bado tunahitaji kilimo bora na chenye
manufaa katika kukuza sekta ya kilimo katika nchi yetu .” Alisema Naibu
waziri Mtumwa
Aidha
alisema changamoto iliyopo hivi sasa ni ukosefu mkubwa wa soko, hivyo
serikali iko mbioni kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Alisema,
iwapo kilimo hicho kitaimarika na kuweza kumnufaisha mtumiaji na mlaji
na kutaweza kupatikana matumaini makubwa kwa kupata kuzalishwa kwa mbegu
ziliobora kwa wakulima waliowengi.
Pia
aliwataka wakulima hao wasivunjike moyo wala wasiwe na wasiwasi na
badala yake wakaze mkanda nayo serikali na taasisi hiyo ya TAHA
itajitahidi kuwatafutia ufumbuzi wa soko la ndani na lanje ili kuweza
kuimarisha zaidi kilimo cha kisasa.
Nae
Mkurugenzi wa TAHA Jaclin Nkinda wakati akitoa nasaha kwa wakulima
alisema kilimo bila ya wanawake haiwezekani kwani wanawake ni wakulima
wakubwa katika kilomo cha mboga mboga na matunda hapa kwetu Zanzibar.
Jaclin
alisema Taasisis ya TAHA ina lengo la kuwasaidia wakulima wa mboga
mboga na matunda kwa nia ya uzalishaji wa mbegu Tanzania bara ili kuleta
na kuendeleza kilimo hicho hapo baadae.
Sambamba na wafadhili,Mfadhili kutoka Finland Tina Huvis alisema Zanzibar inazalisha mboga mboga nyingi ambayo ina lengo la kuisaidi serikali na wakulima wa Unguja ili kufanikisha kilimo cha mboga mboga.
Alisema wafadhili hao wataendeleza mashirikiano yao ili kuleta maendeleo ya kilimo hicho.
Jumuiya
hiyo ilianzishwa mwaka 2004 yenye lengo la kuimarisha kilimo hapa
nchini ikiwa na wadgamini wawili kutoka Filand na USAID
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR