Na Nicholaus Mkoi
Kama hukubahatika kuona watu hawa ambao mara kadhaa tumekuwa tukiwaona kwenye sinema za waigizaji maalum wa Kimarekani kama vile Blus Wills nk utakuwa umekosa uhondo wa aina yake kwani walikuwa vivutia vikubwa sana kwenye Jiji la Dar pamoja na viunga vyake.
Xdeejayz ambayo ilikuwa imemwaga waanahabari wake waliobobea kufanya habari za uchunguzi walibahatika kuwanasa wadunguaji hao" Snipper" wakiwa wamejiachia kwenye majengo marefu wakiimalishga usalama.
Habari zaidi zilieleza kuwa wadunguaji hao hawakuwa Posta peke yake bali kwenye mji mzima wa Dar ambapo Maghorofa yote ya Kariakoo yalijaa wao huku Kigamboni ndo wakiwa wale wenyewe wa kivita kabisa hali iliyzusha hofu na mashaka tele kwa wananchi waliwaona.
Hata hivyo kifaa kilichofungwa kwenye bunduki hizo ambacho humuwezesha mtumiaji kumlenga vyema mlengwa wake na inasemekana vinauwezo wa kufika kilomota kumi umbali wa kutoka Mwenge na Kariakoo.
Habari zaidi zilieleza kuwa wadunguaji hao walifika kwenye sehemu hizo siku tatu kabla ukiacha wale FBI ambao inadaiwa walikuja mwezi mmoja kabla.