Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, July 18, 2013

VIGORI WAMKIMBIA MAIMARTHA,,,,FAHAM ZAID JUU YA HII

Na Imelda Mtema
WASHIRIKI waliokuwa wakiwakilisha  Shindano la Vigori 2013 linaloendeshwa na mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse, Stella Manyanya na Anita James wamemkimbia bosi wao huyo baada ya kuona hakuna kinachoendelea.
Maimartha Jesse.
Akizungumza na paparazi wetu, Stella alisema baada ya kuona siku zinayoyoma pasipo kuambiwa nini kinafuata katika shindano hilo, yeye pamoja na Anita wameamua kuhamia katika Kundi la Classic Girls linalojishughulisha na masuala ya kudansi.
‘Tumeamua kumkimbia Maimartha sababu tulikuwa tukisubiri simu kila siku tunaona mambo hayaeleweki ndipo tukaamua kujiunga na Classic Girls chini yake Monalisa Ivan,’’ alisema Stella.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...