Papa John Paul II atapewa Utakatifu baada ya Vatican kuthibitisha
muujiza wa pili inayosema ulitokea kutokana na sala zake....
Baba Mtakatifu wa sasa Francis I amehakiki muujiza huo, akisema unatoa
nafasi kwa John Paul (pichani) aliyezaliwa Poland kutangazwa Mtakatifu
baadaye mwaka huu.
Vatican.Papa John Paul II atapewa Utakatifu baada ya Vatican
kuthibitisha muujiza wa pili inayosema ulitokea kutokana na sala zake.
Baba Mtakatifu wa sasa Francis I amehakiki muujiza huo, akisema unatoa
nafasi kwa John Paul aliyezaliwa Poland kutangazwa Mtakatifu baadaye
mwaka huu.
John Paul II, aliyezaliwa Karol Józef Wojty a mwaka 1920, alikuwa
kiongozi wa kiroho wa waumini zaidi ya bilioni moja wa Kanisa Katoliki
toka mwaka 1978, mpaka alipofariki mwaka 2005.
Vile vile, Francis I ametangaza pia kumpa utakatifu Papa mwingine, John
XXIII, ambaye aliongoza kanisaKatoliki toka mwaka 1958 hadi 1963
Source: MCL