Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la
Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa yaliyofikia tamati jana kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere
jijini Dar. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara
Dk. Abdallah Kigoda pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dk. Alberic Kacou.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja
wa Wajasiriamali wanaofadhiliwa na UNIDO kwenye banda la Shirika la
Umoja wa Mataifa akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk.
Abdallah Kigoda (kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dk. Alberic Kacou (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga
Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa jijini kwenye viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere leo.
Tuzo
maalum waliyokabidhiwa shirika la Umoja wa Mataifa nchini kwa kutambua
mchango wao wa kuhamasisha Jamii (UN Special recognition for community
awareness) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.