Mazito
yameibuka baada ya msanii mwenye ‘swaga’ za Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, kufungua kinywa na
kusema kuwa ugonjwa wake si bure bali amepigwa kipapai.
Akizungumza
siku ya Juni 28, mwaka huu, Steve alisema kuwa kufuatia kusumbuliwa na
ugonjwa wa ajabu kwa kipindi kirefu sasa na madaktari kushindwa kuelewa
kila walipompima, staa huyo anaamini kuwa amerogwa na msanii mwenzake.
“Nimetembea
kwa wataalamu wa mambo ya asili na kugundua hilo, sasa ninalazimika
kuamini katika imani za kishirikina ingawa ni kitu ambacho muda mrefu
nilikuwa nikikipinga sana lakini kwa hili ninaamini kweli nimechezewa
na ndiyo maana niko hivi hadi sasa,” alisema Steve bila ya kupepesa macho.
“Nashindwa
kumtaja mhusika wa tukio hili kwa sasa ila mwenyewe atakuwa anajua ni
kwa kiasi gani nimemgundua, nimejua kwamba wasanii hatupendani hata
kidogo na wala hakuna anayependa mafanikio ya mwingine.
“Ipo
siku nitamtaja ila leo ngoja niishie kusema kwamba nimechezewa na
namshukuru Mungu kwa kuwa hali yangu inaonesha matumaini ya kupona,” alisema Steve Nyerere.
Hivi karibuni, Steve alivimba mkono wake wa kulia, ilifika hatua alishindwa kulala na kutoka nje kutokana na maumivu.



