MSANII
wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amesema anawachukia sana
wasanii wa kike wa Bongo Movie kutokana na tabia zao za kuchukuliana
mabwana.Amanda
alisema wasanii wengi wa filamu wana tabia za kuibiana mabwana kitendo
ambacho kinamkera na kusababisha kuwachukia kwani wanavyofanya siyo
heshima na inawaharibia sifa kwa jamii pamoja na kuichafua tasnia yao
kwa jumla.
“Nawachukia
na ndiyo maana sitaki kuwa na rafiki Bongo Movie kwa sababu wamekuwa na
tabia mbaya sana mifano halisi ipo lakini siwezi kuitaja,” alisema.
Mbali
na hivyo, Amanda alisema kuna wasanii wawili wa kike walikuwa marafiki
sana hata kwenye mitandao walikuwa wakiitana mawifi lakini hivi sasa
hawaivi, kisa kunyang’anyana bwana.SOURCE GPL




