Kama ule usemi usemao hatujui yatakayo
tokea kesho, ndicho kilichotokea majira ya saa moja jana jioni tarehe
02/07/2013,
baada ya gari dogo lililokuwa linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo
wa Buguruni kumgonga mwenda kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika
maeneo Gereji (garage) Maeneo haya ni mara baada ya kituo cha daladala
Mabibo External, kituo kinachofuata kama unakwenda Buguruni kinaitwa
Gereji, hapa ndipo ilipotokea ajali hiyo
mtu aliyegongwa hakuweza kufahamika kwa wakati huo na mashuhuda wengi wa
ajali hiyo, lakini ni kijana wa kiume mwenye umri kati ya miaka 30 na
22, rangi yake ni mweusi, na alikuwa amevaa t-shirt nyeupe iliyokuwa na
maandishi ya ADIDAS,
Kwa hakika maisha yetu wanadamu ni mafupi sana!! tunaweza kuwa na
mipango mengi na malengo mazuri sana, lakini mwisho wetu ukawa hivi
pasipo hata kutarajia!! ndio maana wale wanao amini juu ya maisha
mengine baada ya kifo, wanfundisha na kusema tunapaswa kujiweka tayari
kiroho wakati wote
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Damu iliyotoka ni nyingi sana
Damu ilimtoka kwa wingi sana mara baada ya ajali katika maeneo ya
kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna kivuko cha waendeo kwa miguu!!
kwa mtazamo usio na uthibitisho wa daktari, kijana huyo alifariki muda
mfupi baada ya ajali. Tunaomba kuchukua nafasi hii kuwakumbusha madereva
wote wazingatie sheria za usalama barabarani, hapa ilipotokea ajali
kuna kivuko cha waenda kwa miguu na pia kuna kituo cha mabasi (daladala)
kwa vyovyote dereva alitakiwa kupungumza mwendo na hata kama pa mtu
anavuka angeweza kumwona na kuepusha ajali. Tunaliomba jeshi la polisi
kitengo cha usalama barabarani, wasichoke kuwaelimisha madereva juu ya
alama za barabarani.
Source: Darubini Leo