Huku
rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela akiendelea kuugua mjini
Pretoria, jamaa zake wamejikuta kwenye malumbano kuhusu mgogoro ambao
umejitokeza wazi kwenye vyombo vya habari.
Badhi
ya jamaa za familia wamemshtaki mjukuu mkubwa wa Mandela, Mandla,
katika juhudi za kutaka kufukua maiti za wanawe watatu wa Mandela ili
wawazike katika makaburi ya Qunu, ambako Mandela anataka azikwe.
Na
Mgogoro kuhusu kutaka kuwafukua wafu hao ni ishara ya mgawanyiko mkubwa
katika familia kubwa ya Mandela, wake zake watatu , watoto sita na
wajukuu 17 na vitukuu
12
. Kulingana na baadhi ya viongozi wa kijamii, wakati familia yake
inapoendelea kuzozana , roho ya Mandela haiwezi kuwa na amani.
Jamaa
kumi na sita wa familia ya Mandela pamoja na viongozi wa kijamii wiki
jana walipewa idhini ya muda na mahakama kufukua maiti hao na kuwapeleka
katika mji wa
Qunu, ambako makaazi ya Mandela yapo.
Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini
Lakini Mandla Mandela, ambaye kulingana na vyombo vya habari, alihamisha maiti hao umbali wa kilomita 22 kutoka mji wa wa Qunu hadi nyumbani kwake eneo la Mvezo mnamo mwaka 2011, anapinga uamuzi huo.
Maiti
hao ni pamoja na Makgatho Mandela, babake Mandla aliyefariki kutokana
na ugonjwa wa ukiwmi, mwaka 2005 pamoja na ndugu zake, Thembekile,
aliyefariki katika ajali ya barabarni na mwanawe wa kwanza aliyefariki
akiwa na miezi tisa, walizikwa kwenye makaburi yaliyokaribiana.
Watatu
hao walifukuliwa bila ya idhini ya familia yote ya Mandela na viongozi
wa kijamii wa ukoo wa AbaThembu ambao pia ni ukoo wa Mandela.
Wanaamini kuwa roho ya Mandela, ina sumbuka hivi sasa kutokana na mzozo kwenye familia yake na ndio maana roho yake haikatiki.
Watu
kumi na sita ni mashahidi katika kesi ya kuomba mahakama idhini ya
kufukua maiti hao, akiwemo mkewe Mandela, Graca Machel, mwanawe Mandela
Makaziwe na viongozi wakuu wa ukoo wa AbaThembu.
Mamia wamekuwa wakikesha kumuombea Mandela apate nafuu
Kinachohojiwa zaidi kwenye mzozo huu ni nani atachukua nafasi ya Mandela kama kiongozi wa familia?
Viongozi
wa kijamii walimteua Mandla kama kijana mwenye umri mkubwa zaidi kuweza
kuchukua nafasi ya Mandela, na kumkabidhi jukumu la chifu Zwelivelile
wa ukoo wa Thembu.
Pia ni mbunge katika chama tawala ANC.
Lakini wengi katika familia wanaonekana kutopendezwa na miendeno yake, akiwemo Makaziwe, mwanawe Mandela wa kike.
Mpango
wake wa kutaka kufungua makavazi katika shamba ambalo makaburi hayo
yapo, imewaacha wengi vinywa wazi katika familia hiyo.
Katika mgogoro mwingine, wanawe wa kike na wakubwa wa Mandela, Makaziwe na Zenani wameenda mahakamani wakitaka kuwanondoa wasaidizi watatu wa Mandela kutoka katika kampuni za baba yao.
Wawili hao wanataka umiliki wa kampuni hizo ambazo ni za thamani ya mamilioni ya dola.
Mjukuu mkubwa wa Mandela , Mandla Mandela
Wiki
jana Makaziwe aliandaa mkutano wa dharura wa kijamii ambapo inasemekana
Mandla alilaaniwa vikali kwa kuhamisha maiti za jamaa zake bila idhini.
Baadhi wanaamini kuwa Mandela lazima asuluhishe mzozo huu kabla ya ya kifo chake.
Moja ya imani za kitamaduni nchini Afrika Kusini ni kuwa mtu huwa hafi wakati ana mambo yanayomsubiri kuyasuluhisha.
Baadhi
wanaamini kuwa badhi ya mambo ambayo bado hajakamilika kwa Mandela ni
kuweza kusuluhisha migogoro hii ndani ya familia pamoja na kuipatanisha
familia take.
Mandela alistahili kuafikiana na familia yake kabla ya kufukua miili za jamaa zake.
Wajumbe wa ukoo wa AbaThembu, wameandaa mkutano wa dharura mjini Qunu baadaye mwezi huu kusuluhisha mizozo hiyo.
BBC SWAHILI