[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI
MNAMO
TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA USIKU HUKO MTAA WA MBATA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. ODEN S/O MKUMBWA, MIAKA 60, MNDALI, MLINZI BINAFSI MKAZI WA NONDE
ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI WAKE NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA KAZINI KATIKA LINDO AMBALO NI DUKA LA
MADAWA MUHUMU [PHAMACY] LILILOPO ENEO HILO. MBINU ILIYOTUMIKA
NI WATUHUMIWA KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA KATIKA LINDO NA KUMUUA KISHA
KUVUNJA DUKA HILO LA DAWA MUHIMU NA KUIBA DAWA ZA AINA MBALIMBALI
PAMOJA NA FEDHA TASLIMU TSHS 600,000/=. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI
WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE.
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO ILIMA BARABARA YA
MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.654 BPX AINA
YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA IMANI S/O MWAKILEMA,MIAKA
34,KYUSA, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAGE D/O
NSUKEMO,MIAKA 59,KYUSA,MKULIMA ,MKAZI WA ILIMA NA KUMSABABISHIA KIFO
CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU
KWA AJILI YA MATIBABU. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA ILEJE - AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA VIFO.
MNAMO
TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBEBE
WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA
MWENDESHA PIKIPIKI T. 863 BXC AINA YA SANYA AITWAE OBADIA S/O
MWAKIPESILE,MIAKA 36,KYUSA,MKAZI WA MBEBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE FRED S/O
FUMBIKA,MIAKA 23,MNDALI,FUNDI UJENZI MKAZI WA ISANGA MBEYA NA
KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MIILI
YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI YA WILAYA YA ILEJE. DEREVA
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI. ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|