Mwigizaji wa kike na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi
amedai kuwa nyimbo yake mpya ya majanga imempa dili la kwenda kurekodi
filamu Afrika ya Kusini, anasema kuwa watayarishaji wa filamu ya Tandeka
iliyorekodi jijini Pretoria kwa kuwashirikisha wasanii watanzania
waishio Afrika ya Kusini imetokana na kufanya vizuri katika muziki hasa
nyimbo yake ya Majanga.
“Uigizaji kwa sasa unachangamoto sana
hilo lilinifanya nirudi katika muziki huku nikichagua filamu za kuigiza
na kujikita katika muziki zaidi ambao unanifanya niwe bussy sana, lakini
ninachofurahia kupitia nyimbo yangu ya majanga nilipoenda kuirekodia
Afrika kusini pia nilipewa uhusika mkuu kuigiza filamu ya Tandeka,”alisema Snura.
Snura anadai kuwa watayarishaji walimuona na kumwita katika usahili
aliposhinda alipewa Script na kuigiza kama mhusika mkuu ambaye aliigiza
kwa umahiri mkubwa filamu ya Tandeka imetumia lugha mbalimbali ikiwa
Kiswahili, Kizulu na Kiingereza, Snura ni msanii mwigizaji wa filamu
aliyetokea katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu.