
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati
nyimbo za Taifa zikipigwa ,wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa
Marekani leo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere .
Nyuma yao ni mama Salma Kikwete na mama Michelle Obama pamoja na mkuu wa majeshi Davis Mamunyange pamoja na IGP Said Mwema .
Kushoto
ni mkuu wa itifaki Balozi Mohamed Maharage na mkuu wa itifaki wa ikulu
ya Marekani ( white House ) balozi capricia Marshall..Ziara ya Rais
Obama inatajwa kuwa moja kati ya ziara za viongozi wan je zilifanikiwa
sana, ambapo pia maelfu ya Watanaznia waljitokeza kumlaki na kumuaga.
![]() |
Rais
Barack Obama akiagama na mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam huku
Mstahiki Meya wa Ilala pamojana Balozi wa Tanzania nchini Marekani
mhe.Liberata Mulamula wakisubiria zamu zao za kuagana na Rais wa
Marekani.
|

Rais
Obama na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One tayari kwa safari ya
kurudi nchini Marekani mara baada ya kumaliza ziara ya siku Mbili
nchini TANZANIA.

![]() |
Rais kikwete na mama Salma Kikwete wakiagana na wageni wao katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere leo .
|

Rais
Kikwete ,Mama Salma na Kikwete,Naibu Waziri wa kilimo mhe Adam Malima
(kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,balozi wa Marekani hapa
nchini Mhe.Alfonso lenhardt wakiwapungia mikono kuwaaga wageni wao
ambao wamemaliza ziara yao ya siku mbili hapa nchini Tanzania baada ya k
ufika jana na kufika ikulu kisha kuongea na Rais wa Tanzania Mhe.DKT
JAKAYA KIKWETE na baada ya hapo alipata fursa ya kuongea na waandishi
wahabari .
NA ISSA MICHUZI BLOG