Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Friday, July 12, 2013

SIPENDI KUONA MVUTANO HUU KILOLO, SASA NI ZAMU YA DC NA MADIWANI YEYE APIGA MARUFUKU MAGARI KULALA MJINI WAO WAJIBU WATAKA AWAPANGIE MAJUKUMU PIA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Bw Joseph Muhumba
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Gerald Guninita
....................................................................................................
KAMA ni mvutano basi huu umezidi wakati mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Gerald Guninita akipiga marufuku magari yote ya Halmashauri ya wilaya ya Kilolo kulala nje ya makao makuu ya wilaya hiyo na kuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Kilolo kuanzia sasa kuanza kuyakamata magari hayo.

Madiwani wamjibu wasema hana mamlaka ya kupiga marufuku hiyo kwani watumishi wa Halmashauri hiyo hawawajibiki kwake na kama anataka wawajibike kwake basi awapangie majukumu ya kila siku.
Pia akishukia chama cha wafanyakazi katika wilaya ya Kilolo kwa kukimbilia kuwatoa taarifa katika vyombo vya habari na kuandika barua .
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa hatua ya chama cha wafanyakazi wilaya ya Kilolo kukimbilia katika vyombo vya habari na kusambaza barua maeneo mbali mbali kulaani hatua yeye kama mkuu wa wilaya kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo alisema ni utovu mkubwa wa nidham kwani ilipaswa wao kama waajiriwa wa Halmashauri ya Kilolo kufikisha madai yao kwa mkurugenzi na si vinginevyo.


Hata hivyo alidai kuwa suala la yeye kutishiwa ameliacha mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kufuatilia jambo hilo hata kama yeye ameamua mkusamehe watu hao

Adai ametumiwa ujumbe wa vitisho na tayari taarifa amezitoa polisi na mkononi ana RB ya taarifa hiyo ambayo ametumiwa kuhusiana na kuwabana watumishi wabadhilifu katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo.


Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo mchana wa leo wakati akitoa maagizo ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.


Alisema kuwa ili kukomesha matumizi mabaya ya matumizi ya fedha za Halmashauri kwa kupelekea watumishi kulala mjini Iringa jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.


“Namwagiza OCD kupitia kauli mbiu ya matokeo makubwa sasa yanawezekana kuwakamata madereva watakao kutwa mjini na magari ya umma”



Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba akizungumza huku akipigiwa makofi na watumishi na madiwani katika kikao hicho alisema kuwa kuna haja ya mkuu huyo wa wilaya na viongozi wengine kuweza kupeana utaratibu wa kuongoza serikali na kuwa kikao kama hicho cha baraza la madiwani ni kikao ambacho kipo kisheria hivyo anapopewa nafasi ya kutoa maagizo ya serikali asigeuze ni sehemu ya kutoa hotuba.



Hivyo alisema kuna haja ya kuelekezana juu ya uendeshaji wa serikali za mitaa na kuwa Kilolo si wilaya changa kama ambavyo mkuu huyo wa wilaya anafikiri na kuwa imefika hapo kutokana na ushirikiano uliopo kati ya watumishi na viongozi na kuwa anashangazwa kuona mkuu wa wilaya anasema kamati ya ulinzi na usalama imesema wakati yeye kama mwenyekiti wa Halmashauri hajui chochote.



Asema kama kila mmoja atakuwa na hali ya vitisho kwa watumishi kazi haitakwenda katika Halmashauri hiyo hivyo kuna haja ya mkuu wa wilaya kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wa Halmashauri hiyo ya wilaya na kuwa kabla yake wapo wakuu wa wilaya ambao wamepita ila wamefanya kazi kwa ushirikiano mkubwa .

Ataka kikao kijacho kiwe na mtiririko mzuri na kama kuna maagizo ya serikali basi mkuu wa wilaya kutumia muda wa dakika 5 kutoa badala ya kurefusha kikao hicho .

Mwenyekiti huyo alisema kuwa hapingi kauli ya mkuu wa wilaya kuwataka watumishi kutokuwa na nidham ya uoga katika kuwatumikia wananchi wa Kilolo

Huku baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo wakidai kuwa mkuu wa wilaya amekosea kupiga marufuku hiyo kwani wao wanawajibika kwa mkurugenzi na si kwa DAS wala ofisi ya mkuu wa wilaya .

Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka watumishi kuwa wavumilivu ya yote wanayotendewa ila wasivunjike moyo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa moyo .

Alisema kuwa jambo kubwa kwa kiongozi ni kuhakikisha anafanyakazi zake kwa kushirikiano na watu hivyo kama kiongozi hatakuwa na ushirikiano basi hakuna litakalofanyika.

Kuhusu uadilifu wa viongozi mwenyekiti Muhumba aliwataka kila mmoja kufanya kazi kwa kujituma zaidi.

Safu hii ya Sipendi kuona baada ya kushuhudia mvutano huu kati ya watumishi wa Halmashauri ya Kilolo pamoja na madiwani dhidi ya mkuu wa wilaya ,unapatwa na maswali mawili matatu ya kujiuliza hivi hadi mkuu wa wilaya anapingwa hivyo ni kwamba hajui wajibu wake? ama watumishi na madiwani hawajui wajibu wao? pia najiuliza watumishi wa Halmashauri wanawajibika kwa mkuu wa wilaya ama kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya ? kama wanawajibika kwa mkurugenzi ni nani yupo sahihi kupiga marufuku magari kulala mjini na je? kwa jografia ya wilaya ya Kilolo hili litatekelezeka?

Swali la mwisho mvutano kama huu ni nani atakayeumia?
SASA SIKIA NASEMA SIPENDI KUONA MVUTANO HUU UKIENDELEA KILOLO
 
 
NA FRANCIS GODWIN - MATUKIO DAIMA BLOG
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...