Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela.
PRETORIA:
Mambo
yanayofanyika katika maeneo matatu ya Afrika Kusini, Hospitali ya
Medclinic alikolazwa, katika makazi yake Mtaa wa Houghton, Barabara ya
Laan 12, Johannesburg na makazi yake ya zamani huko Soweto, yanaashiria
kwamba huenda lolote likatokea kuhusu afya ya Rais wake wa kwanza
mzalendo, Nelson Mandela ambaye kwa siku ya 27 yupo hospitalini akiwa
mahututi.
Baadhi
ya wananchi wamekata tamaa kuhusu afya ya shujaa wao huyo na wanapofika
nje ya Hospitali ya Medclinic, Pretoria alikolazwa, hushindwa kujizuia
na kumwaga machozi.
Baadhi yao wamekuwa wakisema ‘wako tayari kwa taarifa mbaya’ kuhusu kiongozi huyo aliyeongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Mandela
(94) ambaye sasa anatajwa kwa jina la Tata yaani Baba wa Taifa la Afrika
Kusini, amelazwa katika hospitali hiyo ya magonjwa ya moyo na hali yake
inaelezwa kuwa ni mbaya huku taarifa zikisema ‘anapumua kwa msaada wa
mashine’.
Hali
hiyo imewachanganya wananchi wa Afrika Kusini akiwamo Rais Jacob Zuma
na familia ya Mandela ambayo tayari imeingia katika mgogoro mkubwa
unaotafsiriwa na baad
Usiku
wa kuamkia Jumamosi, Mwenyekiti wa Taifa wa Wanawake wa Chama tawala
cha ANC, Baleka Mbete aliongoza maombi ya kumwombea Mandela kwa
wanachama na makada wake waliopo katika Majimbo ya Cape Town na Eastern
Cape huku akisisitiza: “Lazima wananchi wa Afrika Kusini wafike mahali
wamruhusu Mandela ampumzike kwa mapenzi ya Mungu.”
Ukubwa
kwa kishindo cha ugonjwa wa Mandela unaonekana hospitalini Medclinic
alikolazwa, katika makazi yake Mtaa wa Houghton, Barabara ya Laan 12,
Johannesburg na makazi yake ya zamani huko Soweto kwani maeneo hayo
yamekuwa na harakati zisizokoma.
Watu
kwa mamia, wamekuwa wakifika wakiwa wamebeba mabango, kadi, mishumaa na
maua, wengine katika makundi wakiimba, kusoma maneno ya Mungu na
kufanya sala.
Wapo
wanaoifananisha hali iliyopo nje ya kuta za Medclinic na Houghton na
ukuta uliokuwa umezunguka jela alikokuwa amefungwa katika Kisiwa cha
Robben kwa miaka 18 kati ya 27 aliyokaa gerezani.
“Kama
watu walivyokuwa wakikaa nje ya kuta za Gereza la Robben na kupaza sauti
zao kwamba wanataka Mandela aachiwe huru, ndivyo inavyoonekana leo.
Watu wanapaza sauti, wanataka Mandela kutoka ndani ya kuta za
Medclinic,” anasema mmoja wa watu waliokuwa kwenye lango la kuingia
hospitalini hapo.
Kulia mwa
lango hilo lililopo Mtaa wa Celliers, kuna idadi kubwa ya kadi na
mabango ambavyo vina ujumbe mbalimbali kwa ajili ya Mandela, maua na
mishumaa ambayo huwashwa na watu wanaofika sehemu hiyo. Kutokana na hali
hiyo, mtaa huo umefungwa pande zote mbili kwa polisi kuweka vizuizi.
Jumamosi
iliyopita, hofu juu ya afya ya Mandela iliongezeka hasa baada ya kuwapo
kwa pilika nyingi Houghton zilizodumu kwa saa kadhaa, zikiwamo usafi
usio wa kawaida uliojumuisha utengenezaji wa bustani za maua, ufagiaji
wa barabara na matengenezo ya njia za umeme.
Mmoja wa majirani wa Mandela, Jacob Brews alisema harakati hizo si za kawaida na kwamba huenda ‘kuna jambo la ziada’.
Matukio
hayo kwa jumla yake yamevivutia vyombo vya habari vya Afrika Kusini na
vya kimataifa ambavyo vimeweka kambi katika maeneo hayo matatu
yanayoonekana kuwa ni muhimu vikisubiri chochote kitakachotokea.