Watu
wasiopungua 60 wameuliwa katika mashambulio tofauti ya anga
yaliyofanywa na vikosi vya majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani
katika mikoa ya Paktia, Kunar na Helmand nchini Afghanistan. Watu
wasiopungua 45 waliuliwa hapo jana wakati majeshi ya kigeni yalipofanya
mashambulio ya anga katika mkoa wa Helmand ulioko kusini mwa
Afghanistan. Majeshi hayo yanayoongozwa na Marekani yamezidisha
mashambulio ya anga katika maeneo ya raia nchini Afghanistan katika
miezi ya hivi karibuni.
Vifo vya
raia vinavyotokana na mashambulio ya anga yakiwemo ya ndege zisizo na
rubani za Marekani vimekuwa chanzo cha misuguano kati ya serikali ya
Afghanistan na vikosi vya majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani na
kuzidisha pia chuki dhidi ya Washington nchini Afghanistan. Marekani na
waitifaki wake waliivamia Afghanistan mwaka 2001 ikiwa ni katika sehemu
ya kile kilichotajwa kuwa vita dhidi ya ugaidi. Licha ya kuiondoa
madarakani serikali ya kundi la Taliban, machafuko na umwagaji damu
unaendelea kushuhudiwa nchini Afghanistan tangu wakati huo hadi sasa
pamoja na kuweko maelfu ya askari wa majeshi ya kigeni yanayoongozwa na
Marekani