Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (kushoto) katika hafla
maalumu ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi
hilo ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo
imefanyika katika Viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma.
Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba
fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema
Nchimbi kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na
jeshi la Magereza ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma.
Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga,
mjini Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi akitoa hotuba kwa maafisa wa Jeshi
la Magereza kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85
iliyotengenezwa na jeshi hilo. Katika hotuba ake hiyo, Dk Nchimbi
alimshukuru Mkuu wa Jeshi hilo nchini. Kamishna Jenerali John Minja kwa
msaada huo mkubwa ambao utawahamasisha wakazi wa Mkoa wa Dodoma waweze
kufuga nyuki. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza
Kuu Isanga, mjini Dodoma. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.)