Rais Jakaya Kikwete akisikiliza kwa
makini maelezo aliyokuwa akipewa mara baada ya kuingia katika banda la
Umoja wa Mataifa Tanzania lililopo kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini.
Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
Tanzania (UN), Hoyce Temu (kulia), akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete
kusaini kitabu cha wageni baada ya kumaliza kuzungumza na maofisa wa UN
katika banda lao.
Rais Jakaya Kikwete akitia saini kitabu
cha wageni katika banda la Umoja wa Mataifa Tanzania. Kulia ni Ofisa
Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia moja ya
bidhaa za wajasiriamali wanaowezeshwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO)
wakati alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye
maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa nchini akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali kwa kijana
aliyetembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea
jijini Dar.
Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
Tanzania (UN), Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea
banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea jijini Dar.
Wananchi
wakiendelea kumiminika katika banda la Umoja wa Mataifa kupata taarifa
mbalimbali za shirika hilo linavyofanya kazi zake na Serikali ya
Tanzania
Credit: Jestina-George.com