Alisemekana
kuwa katika safari ya kibiashara alipotekwa nyara Novemba mwaka 2011.
"kifo cha mwenzetu Philippe Verdon, kimethibitishwa rasmi,'' ilisema
taarifa kutoka ofisi ya rais Francois Hollande.
"mwili
wake utahamishwa hadi Ufaransa mara moja na kuwa uchunguzi utasaidia
kubaini chanzo cha kifo chake.'' Ufaransa ilituma majeshi nchini Mali
mwezi Januari, ikielezea hofu kuwa wapiganaji wa Al qaeeda huenda
wakavamia mji mkuu Bamako. Kando la hilo, Bwana Verdon na raia wengine
sita wa Ufaransa, wanazuiliwa na wanamgambo wa kiisilamu nchini humo.
Kwenye mahojiano siku ya Jumapili, bwana Hollande alisema kuwa alikuwa
anafanya kila awezalo kuwarejesha wale waliozuiliwa nyumbani haraka
iwezekanavyo.