Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Profesa Tully Kasimoto,
jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya wananfunzi wa mwaka wa tatu
kumfungia ndani ya ofisi yake kwa zaidi ya saa tano wakishinikiza
walipwe fedha zao za kufanyia utafiti.
Sakata hilo lilianza majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya wanafunzi hao kumaliza mitihani yao ya kuhitimu chuo kabla hawajabidhiwa fedha za utafiti, hali iliyowafanya washindwe kuondoka chuoni hapo.
Wakizungumza na gaseti hili kwa sharti la
kutotajwa
majina yao, wanafunzi hao walisema kuwa fedha hizo walipaswa kulipwa
tangu mwezi Mei lakini kutokana na uzembe wa uongozi wa chuo hicho mpaka
sasa hawajalipwa. Sakata hilo lilianza majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya wanafunzi hao kumaliza mitihani yao ya kuhitimu chuo kabla hawajabidhiwa fedha za utafiti, hali iliyowafanya washindwe kuondoka chuoni hapo.
Wakizungumza na gaseti hili kwa sharti la
“Hizo pesa tulitakiwa tupewe tangu mwezi wa tano lakini hadi sasa hatujapewa na kila tunapofuatilia, uongozi wa chuo hautupati majibu sahihi, hali inayotufanya tuishi katika mazingira magumu,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Kwa siku ya jana, wanafunzi hao waliapa kuwa hawatomrumhusu mkuu wa chuo kuondoka kwenye maeneo ya chuo hicho na hata wao hawaondoki mpaka watakapokuwa wamelipwa fedha hizo.
Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kasimoto alipotakiwa kuelezea suala hilo, alikiri kuwa wanafunzi hao walikuwa wakidai fedha zao kwa ajili ya kwenda kufanya utafiti.
Hata hivyo alisema fedha hizo zinapaswa kutolewa na Bodi ya Mikopo na kuwa hadi jana bodi hiyo ilikuwa haijatuma fedha za wanafunzi hao.
Alisema baada ya kuwasiliana na Bodi ya Mikopo alielezwa kuwa fedha hizo ziliingizwa Julai 8, mwaka huu kwenye akauti ya Bodi hiyo aliyoitaja kwa jina la M Bank na kudai kuwa mchakato wa kuhamisha fedha hizo kwenda kwenye akaunti ya chuo iliyo katika benki ya CRDB ulikuwa haujakamilika.
“Taarifa tuliyopewa na bodi ya mikopo ni kwamba fedha ziliingizwa M bank tangu Julai 8, mwaka huu, mchakato wa transaction (kuhamisha) fedha hizo kwenye akaunti ya chuo chetu unachukua siku nne na mpaka sasa fedha hizo bado hatujazipata,” alisema Profesa Kasimoto.
Alisema kuwa wanafunzi hao wamekuwa wakielezwa ukweli huo lakini hawaelewi na hata baada ya kuwataka wachague wenzao watatu ili kwenda kujiridhisha benki hawakukubali.
SOURCE: NIPASHE