Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali Devis Mwamunyange akifungua
rasmi Mkutano wa Makatibu Wakuu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Julai, 2013.
Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Asasi hiyo
utakaofanyika tarehe 13 Julai, 2013.
Baadhi
ya Wajumbe kutoka nchi wanachama wa SADC wakimsikiliza Generali
Mwamunyange (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Kulia
ni Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Usalama nchini Namibia, Bw. Ben
Likando na Bw. Tom Moyane, Kamishina wa Magereza wa Afrika Kusini wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa asasi hiyo. Tanzania ni Mweneyekiti wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC wakati Namibia ni Makamu
Mwenyekiti wa Asasi hiyo na Afrika Kusini ilikuwa Mwenyekiti kabla ya
Tanzania.Picha na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa