Anavyotembea kwa sasa anakutana na watu wengi sana na watu wengi wamekua wakimpigia simu baada ya namba yake kutajwa hewani Clouds FM, wengine amekutana nao njiani na wamekua wakimpa vitu mbalimbali vikiwemo viatu na nguo mpya.
Katoka Mbeya saa kumi alfajiri akafika Makambako saa moja na dakika 19 akiwa tayari katembea kilometa 186, akachukua gari mpaka 92.9 Iringa mjini kwa sababu ilikua imeshakua usiku tayari… akachukuliwa na gari la Wambura mdau wa Power Breakfast ya Clouds FM na kumuacha Iringa mjini alikolala mpaka asubuhi na kuianza safari tena.
Anakwambia saa nane kamili alikua anauanza mlima Kitonga na akaumaliza kwenye saa tisa na dakika kadhaa, baada ya hapo alitembea mpaka kitongoji cha mwisho kabla ya kuianza Ruaha kisha akachukua gari mpaka Morogoro mjini kwa sababu ilikua usiku tayari, ameamkia 88.5 Morogoro mjini na sasa anakuja 88.5 Dar es salaam.
Anasema hii ni idea aliyokua nayo kwa muda mrefu sana lakini akashindwa kuifanya kutokana na kukosa mda ila anamshukuru sana Gerald Hando wa Power Breakfast @Cloudsfm ambae amemsaidia sana kufanikisha hii safari.
Sio sehemu zote anatembea kwa mguu, usiku ukiingia inamlazimu apande gari.