Katika
kile kinachoonekana ni mpango mkakati wa waigizaji wa bongomovies
kujiweka vizuri zaidi kiafya kutokana na ‘’bata’’ nyingi wanazokula,
mwigizaji mwingine wa tasnia hii Jennifer Kyaka ama Odama, naye ameamua
kuingia gym kwa ajili ya kuuweka mwili wake safi zaidi. Katika picha
alizoweka mtandaoni hivi karibuni zilimuonesha mwanadada huyu akiwa
maeneo hayo ya mazoezi na aliandika:
‘’Hizi
ndio harakati za kuweka mwili sawa,Moja ya vitu muhimu katika maisha ya
mwanadamu ni kuhakikisha anafanya mazoezi ili mwili uwe na afya nzuri
so huwa napenda kufanya mazoezi kama hivi...........’’ Kwenye picha hizo
Hii
inakuja baada ya msanii mwingine Vicent Kigosi (Ray) kuamua kuingia
kwenye mchakato wa mazoezi makali sana kupunguza mwili wake ambao wadau
wengi wa bongomovies walisema kuwa haumpendezi.
Hongera sana dada odama!