Na Muhidin Amri–Mbinga,
BAADHI
ya askari polisi wa kituo kikuu Mbinga mjini,wamemtuhumu mkuu wa
polisi wa wilaya hiyo(OCD)Jastine Joseph kuwa ni mtu anayetumia madaraka
yake vibaya kwa kuendesha manyanyaso dhidi ya askari wa vyeo vya chini
na kumuomba Mkuu wa jeshi ilo Said Mwema kumuondoa haraka kabla ya hali
haijawa mbaya zaidi.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa masharti ya kutotajwa majina yao,askari hao
wamelalamika kuwa OCD wao amekuwa akitoa lugha za dharau na hata
zisizopendeza kwao hali inayowavunja moyo wa kazi askari wengine katika
wilaya hiyo.
Walisema,iwapo
jeshi litashindwa kumuhamisha Jastine kunaweza kutokea maafa makubwa
kwani hawatoweza kuvumilia vitendo vinavyofanywa na afisa huyo hasa
ukizingatia kuwa na wao ni watu wakubwa tena wenye familia kama yeye
hivyo kitendo cha kuwatolea lugha za kiuni ni sawa na kuwadhalilisha.
Aidha
wameshauri hata maafisa wengine katika wilaya hiyo wanatakiwa kuondoka
kwani wameshaaka Mbinga kwa muda mrefu hivyo ni vema kupelekwa katika
maeneo mengine ya nchi ili wakapate changamoto mpya za utendaji wa kazi,
na kuendelea kuwepo katika wilaya hiyo ni tatizo kubwa kwani
wameshafahamika na watu wengine hali inayowafanya kushindwa kuchukua
maamuzi sahihi.
Wamesema ocd wao ni mtu hasiyetaka ushauri kutoka kwa mwingine hata kwa maafisa wenzake jambo linalomfanya kutengwa na kujikuta na yuko pekee yake au na wale askari wa kabila lake tu jambo lililowafanya askari kuwepo katika makundi hasa baada ya kufika Jastine kitu ambacho siku za nyuma hakikuwepo na askari wote walikuwa ndugu moja wakiishi na kusaidiana tofauti na sasa.