Obama na Washauri Wake Waandamizi Akiwemo Mark Childress (kulia) |
Rais wa Marekani Barrack Obama amemteua msaidizi wake wa karibu, Mark Childress kuwa balozi wa nchi hiyo, hapa nchini.
Childress
ni msaidizi wa Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) akiwa Naibu
Mkuu wa Utumishi anayeshughulikia mipango katika Serikali ya nchi hiyo
na aliwahi kufanya kazi katika Bunge la Seneti.
Hata
hivyo, taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani jana ilisema nafasi
hiyo inahitaji kuidhinishwa na Bunge la Seneti la nchi hiyo. Uteuzi wake
unaweza kuwa na maana kubwa katika kutekeleza sera za nje za Marekani.
Katika
miaka ya karibuni, Tanzania imeshuhudia ziara za viongozi wakuu wa nchi
hiyo nchini ambao ni Bill Clinton, George Bush na Obama.
Kuteuliwa kwa Childress, kunaashiria kwamba Balozi wa sasa wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt anakaribia kumaliza muda wake.
CHANZO: Gazeti MWANANCHI