Baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uanze, msanii wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka kuwa hachezi filamu za mapenzi kwani zitamsababishia kuharibu funga yake.
Ahojiwa Nisha alisema ndani ya mwezi huu wa Ramadhani hatocheza filamu za mapenzi kwani ni rahisi sana kuharibu swaumu na kujikuta akishinda njaa badala ya kufunga na kumuomba Mungu.
“Kiukweli mwezi huu sichezi filamu za mapenzi kwa sababu huwezi kujua yule mwanaume unayecheza naye anakutamani au la kwani ndani ya mwezi huu ukitamani au ukijiweka katika mazingira ya kutamaniwa tayari umeshamkosea Mungu na kuharibu swaumu hivyo kuepukana na majaribu hayo ndiyo maana nimeamua kuachana na filamu za mapenzi,” alisema Nisha.