Siyo siri
kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny
Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni
namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku ikifika.
Akizungumza
nasi hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya
chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye
maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na
mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi. Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond