Ripoti ya UNAIDS shirika la umoja wa maitaifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi, inasema kwamba kusini na mashariki mwa Africa vifo vinavyosababishwa na maradhi ya Ukimwi vimepungua kwa asilimia 40. Ripoti hiyo inaendelea kusema mataifa kama Botswana, Ethiopia, Kenya, Zambia na Zimbabwe yamepunguza idadi ya watu wanaokufa kwa maradhi ya Ukimwi kwa zaidi ya nusu.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa maradhi nyemelezi ya Kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005.Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi- UNAIDS limehusisha matokeo haya na kutolewa kwa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi kwa wingi barani Africa ndiyo chanzo cha kupungua kwa vifo hivi.
RIPOTI YA BBC.