Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Tuesday, July 30, 2013

Jipya lililosemwa na Serikali kuhusu kodi ya simcard Tanzania

mobile phones 2Gazeti la Nipashe July 31 2013 ndio limemiliki hii post hapa millardayo.com kutokana na habari iliyoandikwa na Gwamaka Apilipi.
Ni kuhusu kauli ya serikali kuhusu ile ishu iliyochukua sana headlines ya kodi ya simcard Tanzania ambapo kwenye Exclusive na Gazeti la Nipashe, Waziri wa fedha katoa ya moyoni.
Anakwambia Serikali imekubali kwamba kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioanzisha kodi hiyo bungeni kwa mjadala zaidi kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao.
Kingine alichosema ni hiki… ‘hili swala kwa sasa linashughulikiwa kwa mapana zaidi na Serikali na linatarajiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, Wabunge watapata nafasi ya kulijadili na muafaka utapatikana’
Nipashe wameandika kwamba wakati hiyo kauli ikitoka kwa Waziri wa fedha, leo utaratibu wa makato ya laini ya simu kwa shilingi elfu moja unatarajiwa kuanza kwa kampuni zote za simu Tanzania.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...