Mwanamke apewa kichapo kikali baada ya kuzini na mchungaji wa kanisa jijini dar
MWANAMKE
anayejulikana kwa jina la Nabii Juliana wa Kanisa la Miracle Assemblies
of God, amepigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa
kuingilia ndoa ya Mchungaji Richard Kiondo. Tukio hilo la
aina yake ambalo lilikusanya umati wa watu, lilitokea hivi karibuni
maeneo ya Ukonga Mazizini, jijini Dar ambapo nabii huyo alipigwa hadi
kuchaniwa nguo. Akielezea
mkasa huo, mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo, Christina Kiondo alisema
baba yake alikuwa akishirikiana kwa huduma ya kanisa na Nabii Juliana
lakini katika ushirika huo anaamini wawili hao walikuwa na uhusiano
usiofaa. Alisema
kisa cha nabii huyo kupigwa, hivi karibuni mwanamke mmoja alikwenda
nyumbani kwa Mchungaji Kiondo na kuwaeleza watoto hao kwamba anamdai
baba yao shilingi 40,000, kitu ambacho kiliwashitua sana kwa kuwa baba
yao anaishi kwa nabii na pia hawakujua fedha hizo alikopa kwa ajili ya
familia gani. Mtoto
mkubwa wa mchungaji huyo, alimtuma mdogo wake nyumbani kwa nabii huyo
kwa lengo la kwenda kumuita baba yao ili aje kuzungumza na mwanamke
huyo. Ilidaiwa kuwa, mtoto huyo alipofika alikutana na nabii na kumwambia amemfuata baba yake lakini alimfukuza. “Baadaye
alikuja hapa nyumbani na kuanzisha varangati kitu ambacho hakikukubalika
kwa majirani kwani tangu siku nyingi wanajua uhusiano wake wa baba. “Majirani
walitoka kwa wingi baada ya kumsikia nabii akitufanyia fujo, walianza
kumshushia kipigo mpaka alipokuja kuokolewa na mjumbe wa eneo hili na
kupelekwa polisi,” alisema Christina. Akizungumza
na mwandishi wetu, mjumbe wa eneo hilo Joseph John ‘Mzee Kasheshe’
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alikiri kutokea kwa tukio
hilo. Kwa upande wake, mke halali wa mchungaji huo ambaye yuko Mbagala kwa matibabu, alisema alizipata taarifa za nabii huyo kupigwa. Aliongeza
kuwa tangu zamani mama huyo alikuwa akienda na mumewe nyumbani hapo
akidhani kuwa wote ni watumishi wa Mungu hivyo hakuwahi kuwatilia shaka
hadi baadaye sana aliponyetishiwa na watu. Kufuatia
kipigo hicho, Nabii Juliana alipofika polisi alitoa malalamiko yake na
kufungua kesi yenye kumbukumbu: MAZ/RB/2246/2013 KUHARIBU MALI. -GPL