WATU wanne wamekufa katika matukio
tofauti mkoani Morogoro akiwemo anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa kifafa
aliyetumbukia mtoni wakati akioga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro , Faustine Shilogile alimtaja aliyetumbukia mtoni ni Emmanuel Maulid (38) mkazi wa Kijiji cha Kichangani , Kata ya Bwakila chini, Wilaya ya Morogoro.
Alisema alikutwa mauti juzi saa 5:30 asubuhi wak
ati akionga baada ya ugonjwa huo aliokuwa nao, kumtokea wakati akioga kwenye mto Mgeta.
Kwa mujibu wa Kamanda alikuwa peke yake hivyo alikosa msaada na ndipo alianguka mtoni na kusombwa na maji. Katika tukio lingine, mtoto mwenye umri wa miaka 10, Twalib Abdalah alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari Julai 12 mwaka huu katika eneo la Bwagala Turiani, Wilaya ya Mvomero akiwa pembezoni mwa barabara.
Aligongwa na gari lenye namba T 6589 BEX Stey Tipa mali ya Kampuni ya CCECC inayojenga barabara ya Magole – Turiani iliyokuwa ikiendeshwa na Patrick Luoga. Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kimetokana na uzembe wa dereva wa gari hilo kutojali watumiaji wengine wa barabara.
Dereva anatafutwa na Polisi. Katika matukio mengine ya Julai 12, mwaka huu Kamanda huyo wa Mkoa alitaja kuwa mwendesha guta, Peter Jorvin (32) alifariki dunia papo hapo saa 11 jioni baada ya kugongwa na gari lenye namba T665 AAF Toyota Cresta iliyokuwa ikiendeshwa na Charles Guwet (26).
Pia Kamanda huyo alisema kuwa katika siku hiyo saa 2 usiku eneo la Uyovi ,Tarafa ya Mikumi katika barabara kuu ya Morogoro –Iringa, mtu mmoja aliyatambuliwa ni Pancras Kisambwe alifariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo pia ilisababisha majeraha kwa abiria mwingine, Khamis Mtupolo (34).
Walikuwa wakisafiri kwa gari lenye namba za usajili T816 BJS Mistubish Fuso ikiendeshwa na Abdu Nyangatuke (33) mkazi wa Ruaha Mbuyuni. Ilikuwa ikitoka Morogoro mjini kwenda Kijiji cha Mololo wilayani Kilosa. CHANZO HABARILEO.