Gazeti
la Wall Street Journal limefichua kwamba, miongoni mwa waliokuwa
wakihudhuria vikao hivyo ni pamoja na Muhammad el Baradei, Amru Mussa na
Hamdin Sabahi. Limesema kuwa katika vikao hivyo kambi ya upinzani
ilitaka kuhakikishiwa kwamba, jeshi litaingilia kati kumuondoa
madarakani Mursi au la.
Maelfu
ya wananchi wa Misri wanaendelea kufanya maandamano katika miji
mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga hatua ya jeshi la nchi hiyo ya
kumuondoa madarakani rais aliyekuwa amechagulwia na wananchi Muhammad
Mursi mapema mwezi huu.